SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, February 4, 2012

Ni Bongo Movie na Wanamuziki wa muziki wa dansi kesho taifa

Na Shakoor Jongo
Pambano la mpira wa miguu kati ya timu ya Bongo Movie na wanamuziki wa muziki wa dansi nchini linatarajiwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Taifa kwa lengo la kuchangisha fedha za waathirika wa mafuliko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzikati jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’ (pichani) alisema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na kinachosubiriwa ni mchezo huo.
“Naamini mechi itakuwa kali sana kutokana na kila timu kujiandaa vema, pesa zitakazopatikana tutawapelekea waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar es Salaam,” alisema JB.
Wakati huo huo, wasanii, Ambwene Yesaya ‘AY’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ wanatarajiwa kugonga shoo kali kesho katika Ukumbi wa New Msasani Club wakati wa uzinduzi wa studio mpya ya Radio Times.
Mkurugenzi wa redio hiyo, Leule Nyaulawa aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, studio itakayozinduliwa kesho ni ile ya B-Hits.

0 comments:

Post a Comment