Afisa Habari wa UN Information Centre (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwakaribisha wageni waalikwa katika semina ya mafunzo kwa vijana juu ya matumizi ya mtandao katika kuhamasisha haki za Binadamu iliyofanyika katika Ofisi za UN Information Centre.
Afisa Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuhusiana na Azimio la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwaka 1948 lenye vipengele 30 ambavyo vimeainisha Haki Msingi za Binadamu na Uhuru.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Elimu kwa Umma wa Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Rosemary Jairo akiwataka wanafunzi kutoa mapendekezo ni namna gani wataweza kusaidia kufikisha ujumbe kiurahisi kwa jamii kuhusiana na Haki za Binadamu ambapo pia amewataka wanafunzi wote waliohudhuria mafunzo hayo kuwa mabalozi katika kutetea haki za Binadamu kama zilivyoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kwa kufikisha ujumbe kwa wenzao na katika jamii inayowazunguka.
Afisa Habari wa United Nationa Information Centre Usia Nkhoma akigawa nakala za Filamu ya "White and Black: Crimes of Color". kwa wanafunzi wawakilishi wa shule zilizohudhuria mafunzo hayo.
Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa kutoka CHRAGG Bw. Ayoub Rioba akielezea nafasi ya vijana kama wahusika wakuu katika matumizi ya Mitandao hiyo ambapo amewataka vijana kuwa watetezi wa haki za Binadamu kwa kutoa taarifa pale wanapoona haki hizo zinakiukwa.
:Mtaalamu wa IT na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu kutoka Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Bw.Wilfred Warioba akielezea jinsi mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano kama vile Facebook, Twitter na Blogs zinavyofanyakazi na zinavyoweza kutumika kupashana Habari na Kuelimishana ambapo pia amesema iwapo itatumika vibaya inaweza kuelta madhara makubwa kwa watumiaji. Katikati ni Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa kutoka CHRAGG Bw. Ayoub Rioba na Afisa Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo.
Afisa Habari wa Temeke Youth Development Network (TEYODEN) Humphrey Shao akifafanua jambo kuhusiana na matumiz ya mitandao kama njia ya mawasiliano.
Mwanafunzi wa Kidato cha Tano Janeth Absalom kutoka Loyola High School akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.
Wanafunzi wakiwa wameshika Poster yenye Ujumbe maalum unaonyesha kwamba Binadamu wote ni sawa bila kujali aina ya Ulemavu mtu alionao.
Afisa Habari wa United Nationa Information Centre Usia Nkhoma akigawa nakala za Filamu ya "White and Black: Crimes of Color". kwa wanafunzi wawakilishi wa shule zilizohudhuria mafunzo hayo.
Pichani Juu na Chini ni Wanafunzi na wageni waalikwa waliohudhuria mafunzo hayo wakitazama filamu "White and Blacks: Crimes of Color" inayozungumzia Maisha, Haki na Adha wanazokabiliana nazo jamii ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albino).
na haki ngowi
0 comments:
Post a Comment