SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, September 11, 2011

SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUTOKA 24 SEVEN 365 (allyshams.blogspot.com/)


Kwa niaba ya wadau wa blogi ya 24 SEVEN 365, Uongozi unapenda kutuma salamu za rambirambi kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete, rais wa Zanzibar, Dk. Ally Mohamed Shein, pamoja na Watanzania wote kwa ujumla popote pale walipo duniani, kufuatia msiba mzito uliolikumba taifa wikiendi hii.

Tumepokea taarifa hizi za kusikitisha kwa mshtuko mkubwa sana, kwani taifa letu ambalo limekuwa katika juhudi za kujikwamua kutoka kwenye umasikini, limepoteza nguvu kazi kubwa sana ambayo ingeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya nchi hii. Hata hivyo, mapenzi ya Mungu nayo hayapingwi. Sisi kama wananchi na taifa kwa ujumla, tuliwapenda sana ndugu zetu waliopoteza maisha katika tukio hilo, lakini Mungu muumba amewapenda zaidi. Na tumshukuru kwa kila jambo.

Kwa upekee kabisa, tunapenda kutoa salamu za pole kwa wafiwa wote huku tukiungana na Watanzania wenzetu katika kuwaombea kwa mwenyezi Mungu muumba kuwapa nguvu za kutosha kuweza kusimama imara katika kukabiliana na majonzi haya. Pia tunawaombea kila lakheri mamia ya wale walionusurika katika ajali hiyo. Tunaamini Mungu atawapa nguvu za kutosha kukabiliana na mshtuko walioupata.
Salamu hizi haziwezi kukamilika bila kuwaomba Watanzania wenzetu kokote kule waliko, kutumia kipindi hiki cha maombolezo kuonyesha mshikamano wetu kwa kuomba dua kwa ajili ya taifa letu ili majanga ya namna hii Mwenyezi Mungu ayaepushie mbali, pamoja na kutupa koyo wa subira wakati mamlaka za nchi zikiwa zinalishughulikia tatizo hili.

"Inna Lillah Waina Illaih Raajiun".

Imetolewa na

Ally S.Mgido's

Founder & Admin


0 comments:

Post a Comment