Rais
Jakaya Kikwete akizindua rasmi mpango mpya wa Bima kwa ajili ya
Watanzania waishio ughaibuni uitwao Welfare Scheme for Tanzanians in
Diaspora (WESTADI).ambapo mwanachama hulipa ada ya dola za Kimarekani
300 kwa mwaka ambazo endapo mwanachama atafariki dunia mwili wake
utasafirishwa na NSSF toka huko aliko hadi nyumbani kwake na pia
msindikizaji mmoja atalipiwa tiketi ya Ndege
Rais
Jakaya Kikwete akihutubia mamia ya Watanzania waishio Marekani wakati
wa kufungua rasmi mkutano wa DICOTA 2011 katika ukumbi wa hoteli ya
Marriott Hotel and Resort kitongoji cha Dulles, Virginia, jijini
Washington DC.
Rais
Jakaya Kikwete akihutubia mamia ya Watanzania waishio Marekani wakati
wa kufungua rasmi mkutano wa DICOTA 2011 katika ukumbi wa hoteli ya
Marriott Hotel and Resort kitongoji cha Dulles, Virginia, jijini
Washington DC.
Wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimshangilia JK wakati nakifungua mkutano wa DICOTA katika ukumbi wa hoteli ya Marriott Hotel and Resort kitongojini Dulles,Virginia, jijini Washington DC. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Bukombe (CHADEMA), Profesa Kulikoyela Kahigi, Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mh Leticia Nyerere, Mbunge wa Liwale Mh. Faith Mitambo (CCM) na Mbunge wa Serengeti Dr Kebwe Stephen Kebwe (CCM)
Sehemu
ya umati wa Watanzania wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete wakati
akifungua rasmi Mkutano wa DICOTA 2011 katika ukumbi wa hoteli ya
Marriott Hotel and Resort kitongojini Dulles,Virginia, jijini
Washington DC
Rais
Jakaya Kikwete akiangalia bidhaa ya mafuta maalumu ya kurutubisha na
kutunza nywele yaliyobuniwa na kutengenezwa na Mtanzania anayeishi
Marekani Bi Lau Kyari kabla ya kufungua rasmi mkutano wa DICOTA 2011 katika ukumbi wa hoteli ya Marriot Hotel
and Resort kitongoji cha Dulles,,Virginia, jijini Washington DC.
Mjasiriamali huyu, ambaye ni Mkemia bingwa, anatarajia kupeleka
Tanzania bidhaa hiyo kabla ya kuanza kutafuta soko la kimataifa
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa washiriki katika mkutano huo
huku Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mh Leticia Nyerere akisubiri
kwa hamu zamu yake baada ya kufungua rasmi mkutano huo katika ukumbi
wa hoteli ya Marriott Hotel and Resort huko Dulles, Virginia, jijini
Washington DC
Rais
Jakaya Kikwete akigombewa kupewa mikono na Watanzania waishio Marekani
baada ya kufungua rasmi mkutano wa DICOTA 2011 katika ukumbi wa hoteli
ya Marriott Hotel and Resort huko Dulles in Virginia, jijini Washington DC.
0 comments:
Post a Comment