SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, September 11, 2011

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA MELI ZANZIBAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Ally Amour wakati alipofika kumjulia hali mtoto Said Gerald (6) aliyenusurika katika ajali ya Meli eneo la Nungwi usiku wa kuamkia jana, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Aliyempakata ni mama yake mzazi, Mariam Hemed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia jana eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia jana eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Baada ya hapo Makamu wa Rais alitembelea katika Viwanja vya Maisala na kutembelea shughuli za kiusaidia na kutambua maiti waliopatikana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwa katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakati alipofika kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia jana  eneo la Nungwi.
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais

0 comments:

Post a Comment