Mwakilishi
wa Tanzania Big Brother Amplified Bhoke Egina (katikati), Kulia ni
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bi. Furaha Sumalu na Kushoto ni
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi.
Barbara
Kambogi akiwasisitiza Watanzania waendelee kupiga kura Big Brother
Amplified japokuwa Tanzania haina mwakilishi. Kulia Bhoke Egina.
Bhoke Egina akishow love na Mdau Othman Michuzi.
The Multichoice Sisters Barbara Kambogi na Furaha Sumalu. “Welcome Back Home”.
****************************************
Watanzania
wametakiwa kutokuwa na mtazamo hasi dhidi ya washiriki pamoja na
shindano la Big Brother na badala yake wawaunge mkono kwa kuwa lile ni
shindano kama menginena zaidi linemjengea mshiriki ujasiri na
kujitambua.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, mmoja wa waliokuwa
wawakilishi wawili wa Tanzania katika shindano la mwaka huu la Big
Brother Amplified Bhoke Egina amesema ushiriki wake umemsaidia kujifunza
mengi ikiwa ni pamoja na kumpa uwezo wa kusoma tabia za watu tofauti na
namna ya kuishi nao na pia kujua uwezo wake mwenyewe wa uvumilivu na
kiwango cha ujasiri.
Mwakilishi
huyo ambaye alitolewa katika jumba hilo kwa kura Jumapili iliyopita
alionesha umahiri wake alipokuwa ndani ya shindano hilo, kwa kuweza
kumudu kukaa kwa wiki tano akiishi na washiriki wengine 26 kutoka
mataifa mbali mbali ya Afrika wakiwemo wa kutoka nchi jirani za Kenya na
Uganda.
Bhoke
ni mwakilishi wa pili kutoka Tanzania kutolewa katika mashindano hayo,
baada ya mwakilishi mwingine Lotus Kyamba kuenguliwa takriban majuma
mawili yaliyopita kwa kuvunja sheria za ndani ya mjengo huo, kufuatia
kumnasa kibao mwakilishi kutoka Afrika Kusini baada ya kutofautiana
kimitazamo.
Naye
Meneja Uhusiano wa Multi Choice Tanzania Barbara Kambogi amesisitiza
umuhimu wa watanzania kuendelea kuwapigia kura washiriki waliobaki ndani
ya jumba hilo, japokuwa Tanzania haina mwakilishi kwa sasa, ili
kuwezesha kufanikisha shindano hilo hadi hatua ya kupatikana kwa
mshindi.
Amesema
kwa sasa upigaji kura ni rahisi, akisema njia ya kwanza ni kwa kutumia
simu ya mkononi kwa mitandao yote isipokuwa ‘airtel’ ambapo unatuma
ujumbe wa maandishi kwa kuandika neno VOTE kisha jina la mshiriki
unayetaka abaki na unatuma kwenda namba 15726 na njia ya pili ni kwa
kutumia mtandao, ambapo kuna website ya Big Brother ambayo ni www.mnetafrica.com/bigbrother ikiingia utaona maelekezo ya jinsi unavyoweza kupiga kura.
Na mo Blog
0 comments:
Post a Comment