Washitakiwa katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Farijala Hussein (kushoto) Rajabu Maranda (kulia) Wakiwa ndani ya gari la Polisi tayari kwa safari ya kwenda rumande kutumikia kifingo cha miaka mitano mara baada ya kutoka kwa hukumu yao leo (jana).
Washitakiwa katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Farijala Hussein (kushoto) na Rajabu Maranda (kulia) Wakiingia kwenye gari ya Polisi tayari kwa safari ya Rumande.
******************
Washitakiwa katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Farijala Hussein na binamu yake Rajabu Maranda, wamehukumiwa miaka mitano jela ambapo pia wametakiwa kurudisha fedha hizo kwa Serikali.
Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na jopo la majaji watatu likiongozwa na Mh. Saul Kinemela. Katika mashitaka yao nane yanayowakabili shitaka la
kwanza lilifutwa kwa kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha hilo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Ilvin Mgeta alisema wamesikiliza na kuzingatia maombi ya upande wa mashitaka katika kutoa adhabu hiyo "Kwa kosa la pili mshitakiwa wa kwanza pekee atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela, kosa la tatu na la nne washitakiwa wote watatumikia adhabu ya miaka mitano, kosa la tano mshitakiwa wa pili pekee atatumikia adhabu ya miaka miwili jela.
"Kosa la sita washitakiwa wote kwa pamoja watatumikia adhabu ya miaka miwili jela na kosa la saba na la nane wote watatumikia adhabu ya miaka mitatu jela," alisema Hakimu Mgeta.Jumla ya miaka ya adhabu hiyo ni 21, ambapo alisema adhabu hizo zitaenda kwa pamoja hivyo washitakiwa hao watatumikia miaka mitano

0 comments:
Post a Comment