SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 11, 2011

UMEPATA KUMSIKIA SUSAN F. MASHIBE HUYU HAPA ANAFUNGUKA!!!

*NI MHITIMU MWENYE SHAHADA TATU IKIWEMO YA URUBANI.
*ANAMILIKI KAMPUNI YA TANJET INAYOSHUGHULIKA NA NDEGE BINAFSI.

Mkurugenzi wa TanJet Hangar Susan Mashibe akilonga na Mo Blog.
Swali : Kama Mo Blog na wadau wetu tungependa kufahamu Susan Mashibe ni nani hasa….?
MASHIBE : Mimi ni mtu complex sana. Lakini labda nianze kwa kuelezea my educational background. Mimi nimesomea uhandisi wa ndege, urubani wa ndege na vile vile management ya ndege. Kwa sasa hivi mimi ni mjasiriamali katika hii sekta ya usafiri wa anga.
Swali : Susan tuambie umeanzia wapi hadi kufikia hapa ulipo..? Kwa maana ya kwamba ilikuwa ni mipango yako kusomea masomo hayo au hali ya maisha imekufanya ukajikuta katika fani hii..?
MASHIBE : Nilikuwa na nia ya kutaka kurusha ndege tangu nikiwa na miaka minne.Mapenzi yangu kwa ndege yalianza wakati wazazi wangu na mimi tulikuwa tunaishi Kigoma. Kipindi Fulani wazazi wakawa wanasafiri kutoka Kigoma kuja Dar es Salaam. Wakaondoka na wadogo zangu wawili, mimi wakaniacha na bibi ambaye alikuwa amekuja kuniangalia. Ndege ilipokuwa inaondoka roho iliniuma sana, nikasema ningekuwa naweza kurusha ile ndege wasingeniacha. Kwa hiyo nikapata hamu sana ya kurusha ndege ili siku nyingine wasiniache. Kipindi hicho niko na miaka minne lakini sikuwa yule mtoto wa kulia lia kwamba nimeachwa na mama, mimi nilikuwa mtoto wa kufikiria sana, huwa nafikiria, nasema nataka kitu fulani, kweli siogopi nakiendea na nafanikiwa.
Swali : Kutokana sasa na nia uliokuwa nayo. Tufahamishe ulianzia wapi kielimu mpaka kufikia kutimiza malengo yako ya urubani wa ndege..? 
MASHIBE : Nilipomaliza form four nilichaguliwa kwenda chuo cha ualimu, lakini mapenzi yangu yalikuwa kwenye ndege. Yani kulikuwa hakuna kitu kingine nilikuwa napenda nifanye zaidi ya ndege. Wakati huo tayari dada yangu alikuwa yuko Marekani, kwa hiyo nikapata nafasi ya kwenda Marekani kusoma. Maana baada ya kumaliza form four mimi sikusoma form five wala six. Nilimaliza Pamba Sekondari pale Mwanza baada ya hapo nikaenda Marekani.
Na nilipofika kule nilikuwa siwezi hata kuongea kiingereza na ili uweze kurusha ndege ni lazima u-communicate na control tower kwa kiingereza. Hivyo mwalimu wangu akanishauri kabla hawajaniruhusu kwenda solo (Solo ni kuruhusiwa 
kurusha ndege peke yako bila mwalimu, ukiwa na mwalimu inaitwa duo) nijifunze kwanza kujieleza na kuongea. Nikaona hiyo itanichukua muda. Nikasema wakati najifunza kuongea pia nataka nijifunze kila kitu kuhusu ndege. 
Na kulikuwa na chuo cha uhandisi wa ndege karibia na kule nilikokuwa naishi. 
Nikaenda nikajiandikisha. Nikasema nataka kusoma uhandisi wa ndege, kwa sababu nilijua mimi nilikuwa napenda sana masomo kama Physics na hesabu hivyo nikajua darasani theory haitanisumbua sana. Kwa sababu hesabu ni numbers hazina lugha na kama ni laws za physics ni laws tu. Nikaju pia nitachukua madarasa ya kuongea English. Nikajikuta mpaka nakuwa fluent in English tayari nimeshamaliza masomo yote ya uhandisi na nikafanya mtihani wa taifa wa uhandisi wa Marekani wa Civil Aviation yao inayoitwa FAA. Nikapass na nikajikuta nimekuwa mhandisi japo haukuwa mpango wangu kuwa mhandisi. Sasa kutokana na gharama za mafunzo ya ndege kuwa kubwa ilibidi nifanyekazi kama mhandisi ili niweze kujilipia mwenyewe mafunzo hayo. 
Nikawa nafanyakazi usiku ya kutengeneza ndege mchana na kwenda kurusha. Ili uweze kukaa kule inabidi kujiandikisha kuwa mwanafunzi fulltime hivyo nikalazimika kujiandikisha na nikajikuta nasoma Aviation Management. Kwa hiyo mazingira kwa ujumla yakasababisha mpaka nilivyokuja kumaliza vyote nimekuwa Mhandisi, Rubani na Meneja wa Mambo ya Ndege.
Susan Mashibe akifanya mahojiano na Lemmy Hipolite wa Mo Blog.
Swali : Imekuchukua muda gani/miaka mingapi mpaka kumaliza vyote hivyo..?
MASHIBE : Ahhh…!! Imechukua muda mrefu maana nimekwenda Marekani mwaka 93. Uhandisi, Urubani na Management nimechukua kama miaka 9 na hizo ni Degree Tatu tofauti. Wakati huo gharama za kurusha ndege ilikuwa ni kama dola 90 ($90) kwa saa hivyo nilikuwa narusha kwa saa 2 kwa wiki kutokana na uwezo wa kifedha, kwa sababu nilikuwa natengeneza kama $ 12 tu kwa saa na natakiwa kulipia kurusha ndege, manejiment, kodi, gari, mafuta na mahitaji mengine hivyo nikalazimika kufanya kazi saaana. Nilipata leseni yangu ya kwanza mwaka 2000 na ya pili mwaka 2001 na ya tatu mwaka 2002.
Swali: Ulipomaliza masomo na kuhitimu ulianza kufanya kazi Marekani moja kwa moja? Na ilikuaje ukarejea nyumbani Tanzania..?
MASHIBE : Kama nilivyosema mwanzo nilipojikuta nimekuwa mhandisi nililazimika kufanya kazi kama mhandisi ili nipate fedha za kulipia masomo niliyokusudia ya urubani. Na lengo langu nilitaka nikafanye kazi ya kurusha ndege katika mashirika makubwa kama Delta, kwa sababu nilitaka kurusha ndege aina ya Boeing 777. Sasa Napata leseni yangu mwaka 2001 wakati namalizia masomo nadhani kila mtu anakumbuka kilichotokea ile September 11 hali iliyopelekea industry ya ndege kuvurugika. Hata hiyo Delta yenyewe niliyotaka kwenda ililazimika kupunguza marubani hivyo nikagundua siwezi kupata kazi ndipo nikaanza kufikiria kurudi nyumbani.
Ilinichukua miaka miwili kutafuta kazi nyumbani na hakuna mtu aliyekuwa tayari kuniajiri. Lakini mwaka 2003 nikaamua kujiajiri mwenyewe hivyo I set my mind kuwa I will make it happen in Tanzania na hii yote ni kwa sababu ya mapenzi ya kazi hiyo. Nilikuwa naweza kubadili fani labda niingie katika media au nikabakia Marekani lakini nikasema hapana nakwenda Tanzania na nitafanya vitu vyangu.
2003 nikaanzisha kaofisi kangu ambapo mpaka leo kako pale uwanja wa ndege wa Dar. Nikaenda kuomba kupata hangar yaani eneo kubwa ambalo tunaweza kuweka hata ndege ndani, nikawaeleza what I want to do, wakaniambia kwanza sisi hata hatuelewi unaongea kitu gani.
Kwa kifupi mwanzo ulikuwa mgumu kwa sababu ile sector ambayo mimi nilikuwa nime specialize ya ndege binafsi huku ilikuwa haipo. Watu walidhani mimi nikichaa, wakaniambia kama unataka biashara ya aina hiyo nenda Nairobi.
Habari zaidi:
Click

0 comments:

Post a Comment