SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 11, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA, ISTANBUL LEO

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Anna Tibaijuka, wakati wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya Nchi Masikini, unaoendelea jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo unatarajia kumalizika Mei 13 mwaka huu. 
 
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Anna Tibaijuka akiteta jambo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), Jacques Diouf, wakati walipokutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo kwenye Ukumbi wa Mkutano jijini Istanbul leo Mei 11. 
Makamu wa Rais Dkt Bilal, amemuwakilisha Rais Jakaya kikwete katika Mkutano wa  Umoja wa mataifa kuhusu Maendeleo ya nchi masikini, unaoendelea jijini Istanbul.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), Jacques Diouf, wakati walipokutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo kwenye Ukumbi wa Mkutano jijini Istanbul leo Mei 11.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
Chanzo: H@ki Ngowi 

0 comments:

Post a Comment