SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 18, 2011

SIMBA NA WYDAD KUCHEZA CAIRO!!!

Kikosi cha timu ya Simba.


Kikosi cha Wydad Casablanca ya Morocco.
Mechi ya kutafuta timu itakayocheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco itachezwa Mei 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Petrosport jijini Cairo, Misri. Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) liliamua mechi hiyo ya mkondo mmoja ichezwe uwanja huru (neutral ground).
Iwapo muda wa kawaida wa dakika 90 utamalizika kwa sare, mshindi atapatikana kwa mikwaju ya penalti. Wenyeji wa mechi (kwa maana ya kupokea timu na viongozi uwanja wa ndege) ni Chama cha Mpira wa Miguu cha Misri (EFA).
Gharama nyingine zozote zitabebwa na timu husika kupitia vyama vyao-Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF).
Kila timu itajigharamia usafiri wa kwenda Cairo, pamoja na gharama za malazi. EFA imeombwa kusaidia timu zote katika maandalizi ya hoteli za kufikia.
Gharama za maofisa wa mchezo (waamuzi na kamishna) ikiwemo usafiri na malazi zitabebwa na klabu hizo kupitia vyama vyao (TFF na FRMF). Gharama zozote ambazo EFA itatumia katika maandalizi ya mechi hiyo zitarejeshwa na TFF na FRMF.
Pia mapato yatakayopatikana kutokana na viingilio katika mechi hiyo, EFA itayagawa nusu kwa nusu kwa klabu hizo kupitia vyama vyao vya mpira wa miguu- TFF na EFA.
Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF.

0 comments:

Post a Comment