Mchungaji wa kanisa moja huko California Marekani, Harold Camping,
ametabiri kuwa Mei 21,2011 saa moja kamili usiku mwisho wa dunia, na
huenda tusiione tena jumapili ya wiki ijayo, kwani dunia itakuwa imefika
mwisho wake siku hiyo ya Jumamosi.
Mchungaji Camping kwa kutumia mahesabu ya tarehe na mafunzo ya
Biblia, ametabiri kuwa kiama kitakuwa jumamosi, na miezi mitano baadae
kwenye tarehe 21 Oktoba, Mungu ataiteketeza dunia.
Mchungaji Camping ambaye anamiliki radio ya Christian Family Network
yenye mtandao mkubwa sana nchini humo na sehemu zingine duniani ikiwa
inarusha matangazo kwa lugha zaidi 48 zikiwemo lugha kutoka Afrika
Kusini.
Camping mwenye umri wa miaka 89 ana wafuasi wengi sana duniani na
sasa anaendesha kampeni kubwa kuwajulisha watu kuhusu mwisho wa dunia
hapo Mei 21.
Magari yenye mabango yenye ujumbe mwisho wa dunia Mei 21 yamekuwa
yakionekana sehemu mbalimbali za Marekani yakitangaza kuwa mwisho wa
dunia ni Mei 21 kwa sababu itakuwa ni siku ya 722 500 tangu Yesu
aliposulubiwa msalabani mnamo Aprili moja AD33.
Aidha Mchungaji Camping amesisitiza kuwa kuwa namba 722 500 ni
muhimu sana kwa wakristo duniani kwani inapatikana kwa kuzizidisha namba
tatu tukufu (5, 10, 17) mara mbili {5x10x17x5x10x17}
Hii sio mara ya kwanza kwa mchungaji Camping kutabiri matukio makubwa
duniani coz Septemba 6 mwaka 1994 akiwa na wafuasi wake wengi
walikusanyika mbele ya ukumbi wa Alameda wakisubiri kurudi kwa Yesu
Kristo ambaye hakutokea na tangu wakati huo,camping amesema kuwa
wamefanya utafiti mkubwa sana na hivyo wana uhakika safari hii utabiri
wao utakuwa sahihi.
0 comments:
Post a Comment