UPEPO wa kisiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), unazidi kuvuma kwa kasi baada ya Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Wilson Mukama, kutangaza kiama kwa mafisadi akitaka wajiuzulu mapema, huku Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Chama hicho, Makongoro Nyerere akitajwa kuchochea maamuzi magumu dhidi ya genge hilo.
Kauli hizo nzito za vigogo hao dhidi ya genge la mafisadi ambalo lina nguvu za fedha ndani na nje ya chama hicho tawala, ni sehemu ya mpango mkakati wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, wa kukivua magamba.
Mukama ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa chama hicho aliyetangazwa mjini Dodoma usiku wa kuamkia jana, alisema ili chama hicho kiweze kurudisha heshima yake kinatakiwa kuwa na watu safi wasiotiliwa mashaka kabisa katika jamii.
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake muda mfupi baada ya kumaliza kikao na watendaji wa mikoa wa chama hicho, Katibu huyo alisema hana jipya atakalopeleka CCM isipokuwa yeye atasimamia weledi na misingi iliyokuwapo tangu kuanzishwa kwa CCM.
“CCM inatakiwa kujengwa upya kabisa na ili hayo yaweze kufanikiwa, kuna kila sababu za kuwa na watu safi, hivyo mimi nawataka ndugu zangu wasimame katika misingi ya zamani tuliyokuwa nayo katika chama chetu,” alisema Mukama na kuongeza:
“Nawataka wote wenye tuhuma za rushwa na ufisadi ndani ya chama waanze kujiuzulu mapema ili kulinda heshima yao, kwani tunaingia kujenga chama sio kukibomoa.”
Katibu Mkuu huyo ambaye ana kibarua kigumu cha kusafisha chama na kukirejesha katika misingi ya waasisi wake tangu enzi TANU na CCM ya mwaka 1977, alisema mwelekeo wa CCM pamoja na sera zake bado unakubalika kwa wananchi na kuongeza: "Kinachotakiwa sasa ni kuwa na usimamizi na maamuzi magumu kwa kila mtu atakayekabidhiwa dhamana hiyo".
Akizungumzia juu ya chama kujengwa upya alisema: "Ili tuweze kufanikiwa katika hilo mimi nitasimamia maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM ya kukirudisha chama kwa wanachama ngazi ya chini ili wao ndio wakafanye maamuzi.”
Mukama ambaye alikuwa akizungumza kwa kujiamini alisema atasimamia kikamilifu itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea, kwa kuwa ndio sera kubwa ya CCM tangu kuanzishwa kwake.
Habari Zaidi: BOFYA

0 comments:
Post a Comment