Na.MO BLOG TEAM
Kamati ya Kimataifa inayofanya mashauriano na waasi wa Libya imemtaka kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi kusimamisha mapigano na kuondoka madarakani mara moja ili kujenga mazingira ya kupatikana kwa suluhisho la mgogoro wa Libya kwa njia ya mazungumzo.
Wajumbe wa kamati hiyo wametoa wito huo baada ya mkutano wao wa mjini Doha uliohudhuriwa pia na wawakilishi wa Baraza la Kitaifa la waasi wa Libya.
Wajumbe hao kutoka nchi karibu 20 na mashirika ya kimataifa wamesema kuwa Kanali Gaddafi kuendelea kuwepo madarakani kutakwamisha juhudi za kutatua mgogoro wa nchi hiyo.
Washiriki wa Mkutano huo pia wametoa taarifa kuwa wanachunguza uwezekano wa iwapo fedha za utawala wa Gaddafi zilizozuiwa katika mabenki ya nje zinaweza kutolewa kwa wapinzani.
WAKATI HUO HUO
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Jumuiya ya kijeshi ya NATO leo wanakutana mjini Berlin kujadiliana juu ya mustakabal wa Libya baada ya kutokea mzozo miongoni mwa nchi hizo juu ya utekelezaji wa hatua za kijeshi ili kuwalinda raia nchini humo.
Nchi za Ufaransa na Uingereza zimeilaumu Jumuiya ya NATO kwa kutofanya vyakutosha katika kuzitekeleza hatua hizo.
Nchi hizo zinataka mashambulio ya kijeshi dhidi ya majeshi ya Gaddafi yaimarishwe.

0 comments:
Post a Comment