Vikosi vya usalama nchini Syria vimewaua waombolezaji watatu wakati walipofyatua risasi katika mazishi ambayo yaligeuka kuwa maandamano kaskazini mwa mji wa Homs.
Maelfu ya waombolezaji walihudhuria mazishi mtu mmoja aliyeuawa siku moja kabla na vikosi vya serikali kisha waliandamana hadi eneo walipokuwepo polisi na watu wenye silaha wanaomtii Rais Bashar al-Assad hivyo kusababisha mauaji hayo.
Mauaji hayo yamefanyika siku moja baada ya Rais Assad kusema kuwa serikali itaondoa sheria ya hali ya hatari ambayo ilipitishwa tangu mwaka 1963.
Sheria hiyo inazuia mikusanyiko ya hadhara na inaruhusu mtu kuhojiwa wakati wowote na kufuatilia mawasiliano binafsi.
NCHINI YEMEN
Maandamano makubwa yamefanyika kwenye mji mkuu wa Yemen wa Sanaa huku vikosi vinavyoipinga serikali vikitaka Rais Ali Abdullah Saleh kuondoka madarakani.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa vikosi vinavyomtii Rais Saleh vilifyatua risasi kwa waandamanaji ambapo watu wanne wamejeruhiwa.
Waandaaji wa maandamano hayo wamesema kuwa waandamanaji pia wameingia mitaani kwenye miji ya Taez na Ibb iliyopo kusini mwa nchi hiyo na mji wa Al-Hudaydah.
Takriban watu 100 wameuawa na maelfu wengine wamejeruhiwa tangu vuguvugu la vijana wa Yemen lilipoanza katikati ya mwezi Februari mwaka huu wakipinga utawala wa Rais Saleh wa miaka 32 madarakani.
Na Mo Blog

0 comments:
Post a Comment