MSIBA HYDERABAD-INDIA
TANZANIA STUDENT ASSOCIATION HYDERABAD
Jumuiya ya wanafunzi wa Kitanzania Hyderabad India kwa masikitiko makubwa mno inatangaza kifo cha mwanafunzi SHAKIR HADOUN MARHUBI kilichotokea India.Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu popote walipo.Taratibu za mazishi zinapangwa.
Marehemu shakir Hamdoun Al-marhubi wakati wa uhai wake.
Marehemu alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu akisoma kozi ya BCA katika chuo cha Osmania kilichoko hapa hyderabad,mwili wa marehemu ulikutwa nyumbani kwake alipokuwa anaishi taarifa za kifo chake hazijajulikana hadi sasa,mwili wa marehemu umehifadhiwa Gandhi hospital.

Marehemu mwenye Tisheti nyekundu akiwa na rafiki zake hapa hyderabad
Marehemu wa pili kutoka kulia enzi za uhai wake hapa akiwa uwanjani masab tank
Marehemu enzi za uhai wake ..akiwa na goli kipa wa timu ya wanafunzi TSAH ..NA M/KITI MSTAHAFU WA TSAH Bw Nkya
Watatu kutoka kushoto kwako ..akiwa kwenye sherehe ya mahafali ya wa wanafunzi tsah
Mkiti mstahafu TSAH Bw,Nkya akiwa msibani sainikpuri
Mkiti wa kamati ya starehe TSAH mstahafu mwenye aliyevaa shati nyekundu alikuwepo kwenye mazishi na ndie aliyetayarisha hizi picha ...
Mwenye fulana nyeusi ktkt Mr Abdul Aziz ndie alikuwa mtu wake wa karibu sana
Msibani sainikpuri
Aliyesimama ni sheikh Mohammed Best akitoa mawaidha kwenye msiba
Hii ndio nyumba Wanajumuiya walipokutana kupanga taratibu za mazishi
Kwa kweli wanafunzi walikuwa ni wenye simanzi mno
Walijitokeza wanafunzi wengi sana ,kuonesha kuwa bado wanampenda ndugu yao.
TULIKUPENDA SANA NDUGU YETU LAKINI MWENYEZI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI.
SISI WOTE NI WA M/MUNGU NA KWA HAKIKA KWAKE TUTAREJEA.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi
TULIKUPENDA SANA NDUGU YETU LAKINI MWENYEZI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI.
SISI WOTE NI WA M/MUNGU NA KWA HAKIKA KWAKE TUTAREJEA.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi
AMIN.
0 comments:
Post a Comment