HAFLA YA SOMESHA MTOTO WA KIKE YAFANA

Mgeni
rasmi kwenye hafla ya kuchangisha pesa za mpango wa Somesha Mtoto wa
Kike (SOMKI) inayoandaliwa kila mwaka na Unity of Women Friends (UWF)
Mama Margaret Chacha, Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania
(TWB), akitoa hotuba wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa
Kibo hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar usiku wa kuamkia leo

Mama Margaret Chacha akizindua
tovuti ya UWF kwenye hafla hiyo

Mshereheshaji Baby Madaha akitangaza kwamba jumla ya shilingi milioni 47 zimepatikana katika hafla hiyo ya hisani ya SOMKI

Mama Margaret Chacha akitangaza washindi
wa bahati nasibu iliyochezeshwa

Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo

wadau mbalimbali kwenye hafla hiyo

Meza ya kampuni ya mafuta ya TOTAL ilisheheni vilivyo

Mnunuzi
wa picha ya mtoto wa kimasai (mwenye buluu) akikabidhiwa mzigo wale
alioununua kwa dola za kimarekani 1,500 katika mnada uliopitishwa kwenye
hafla hiyo

Mshindi wa simu ya Nokia na muda wa maongezi wa shilingi 50,000 akikabidhiwa zawadi yake baada ya kushinda bahati nasibu

Mdau akifurahia zawadi ya blender toka Mini Argos aliyoshinda kwenye bahati nasibu

Mama Chacha akiwa na wana UWF baada ya kuzindua tovuti yao

Meza
kuu pamoja na wanachama wa UWF na waume zao. Walioketi toka kulia ni
Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngereja, akifuatiwa na Gavana wa
Benki Kuu Profesa Benno Ndullu na mgeni rasmi Mama Margaret Chacha




0 comments:
Post a Comment