Wachunguzi wapongeza uchaguzi wa Guinea
Mgombea Urais Alpha Conde Kulia), kiongozi kwa ajili ya Rassemblement
Wachunguzi wa kimataifa wamepongeza jinsi uchaguzi wa jana jumapili ulivyoandaliwa nchini Guinea kwa njia ya amani.
Ujumbe wa wachunguzi hao kutoka umoja wa Afrika na umoja wa Ulaya umesema duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa urais imeshuhudia idadi kubwa ya raia wakijitokeza kupiga kura.
Wachunguzi hao wamewataka wagombea wawili katika uchaguzi huo Cellou Dalein Diallo na Alpha Conde kuwa watulivu hadi pale matokeo yatakapotangazwa.
Duru ya pili ya uchaguzi huo iliahirishwa mara mbili kutokana na machafuko yaliyoibuka kati ya wafuasi wa wagombea hao.
Guinea imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu mapinduzi yaliyofanyika miaka miwili iliyopita
0 comments:
Post a Comment