SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, November 2, 2010

Baada ya Shein kuangazwa mshindi, Maalim Seif atoa mwito wa mshikamano Zanzibar

Maalim Seif wa CUF (kulia), akimpongezaDk. Shein baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi ya Urais Zanzibar 2010, matokeo yaliyotangazwa na Tume Ya uchaguzi ya Taifa Zanzibar usiku wa kumakia leo.

Ni wakati wa muafaka na kuungana
Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF nchini Tanzania amewataka Wazanzibar wadumishe umoja na mshikamano na walinde maridhiano yaliyofikiwa fisiwani Zanzibar.

Matamshi hayo ya Maalim Seif yamekuja baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kumtangaza mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar kwa kupata asilimia 50.1 ya kura za uchaguzi mkuu wa siku ya Jumapili ya Oktoba 31. 

Kwa mujibu wa mabadiliko ya hivi karibuni ya Katiba ya Zanzibar, sasa Maalim Seif Sharif Hamad aliyepata asilimia 49.1 ya kura katika uchaguzi huo, atakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi mkuu Zanzibar kufanyika kwa amani na utulivu kiasi kwamba baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo na licha ya kuweko malalamiko mengi, lakini Katibu Mkuu wa CUF maalim Seif Shariff Hamad amekubali haraka matokeo hayo hatua ambayo wachambuzi wa mambo wanahesabu kuwa ni ya hekima kwa ajili ya kuepusha machafuko na umwagikaji wa damu katika visiwa hivyo vilivyo na historia mbaya ya machafuko ya kabla, wakati na baada ya uchaguzi. 

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, baada ya kutangazwa matokeo hayo, Maalim Seif alikubali kutoa hotuba ambayo ilijaa hekima na busara ikieleza umuhimu wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande mbili kuu Zanzibar, huku akitaharisha kuhusu vitendo vinavyoweza kuvuruga maridhiano hayo.

0 comments:

Post a Comment