SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 27, 2010


UN yaitaka Marekani iondoe vikwazo vyake vya miongo mitano dhidi ya Cuba

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha kwa wingi mkubwa mno wa kura azimio la kuitaka Marekani iondoe vikwazo vyake vinavyoendelea kwa muongo wa tano sasa dhidi ya Cuba. Azimio la 19 la kila mwaka la kulaani vikwazo hivyo liliungwa mkono na nchi 187 wanachama wa Umoja wa Mataifa na kupingwa na Marekani na Israel tu. Nchi nyingine tatu ndogo ambazo ni waitifaki wa Marekani ziliamua kutopiga kura. Awali vikwazo hivyo viliwekwa kwa namna isiyo kamili katika mwaka 1960 baada ya mapinduzi ya Cuba yaliyoongozwa na Fidel Castro, na hatimaye kutekelezwa katika sura ya sheria kamili mnamo mwaka 1962 na ndilo baki kuu katika mabaki ya enzi za Vita Baridi. Marekani imeweka marufuku ya biashara na safari nyingi za kuelekea Cuba. Licha ya matamshi aliyotoa mwaka jana Rais Barack Obama wa Marekani wa kuanzisha kile alichokiita ‘mwanzo mpya' na Cuba Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Bruno Rodriguez ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa vikwazo vya Washington dhidi ya nchi yake ‘vimeshadidishwa' katika mwaka huu. Kwa mujibu wa Rodriguez vikwazo hivyo vya miaka 50 vimeigharimu Havana jumla ya dola bilioni 750 na kwamba hatua hiyo ya Marekani ni ya vita vya kiuchumi na mauaji ya kimbari. Amesisitiza kuwa inachotaka Washington ni kuwepo nchini Cuba serikali kibaraka inayoiunga mkono suala ambalo amesema halitotokea..

0 comments:

Post a Comment