SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, October 7, 2010

Clinton: Washington ijiweke tayari kupoteza nafasi yake ya kuudhibiti ulimwengu
Bill Clinton, Rais wa zamani wa Marekani amesema, kutokana na kuongezeka nguvu za nchi kama vile China na India, Marekani ijiweke tayari kupoteza nafasi yake ya udhibiti wa ulimwengu. Bill Clinton alinukuliwa hivi karibuni, katika kikao cha saba cha kila mwaka cha Stratijia ya Ulaya ya Yalta kilichofanyika nchini Ukraine akisema kama ninavyomnukuu:" Wakati uchumi wa nchi nyingine unapiga hatua mbele zaidi kuupita uchumi wetu bila ya shaka nchi hizo zitataka kuongeza nguvu zao za kijeshi pia na hivyo hazitokuwa tena na utegemezi kwa Marekani," mwisho wa kumnukuu. Huku akielezea matumaini yake juu ya Washington kuendelea kuwa na taathira katika kujenga ‘daraja la urafiki na mataifa mengine' Clinton amesisitiza kuwa ikiwa Marekani inataka ipige hatua mbele lazima ikubali kuachia na kupoteza baadhi ya fursa ilizonazo hivi sasa

0 comments:

Post a Comment