PPF Yaipiga Jeki Hospitali Ya Temeke, Yatoa Msaada Wa Matanki Ya Kuhifadhia Maji Kupunguza Kero Wodi Ya Kinamama
Afisa kanda wa PPF Temeke, Lindi na Mtwara Bi. Linda Njoolay akigawa sehemu ya msaaada kwa wagonjwa wa hospitali ya temeke. Kulia Dk. Asha Mahita, Mganga mkuu hospitali ya Temeke.
Meneja wa PPF kanda ya Temeke,Lindi na Mtwara Bi.Lulu Mengele (wa pili kulia)akikabidhi stakabadhi ya malipo ya mantanki ya maji kwa mganga mkuu wa wilaya ya Temeke Dk. Asha Mahita. Matanki hayo yatasaidia kutatua tatizo la maji hospitalini hapo hasa katika wodi ya kinamama na chumba cha upasuaji.Pembeni kulia ni Meneja wa mahusiano wa PPF Bi.Sarah Kibonde Msika. PPF imefungua kanda mpya wilayani Temeke ili kusogeza huduma karibu na wanachama wake
Wafanyakazi wa PPF wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Temeke, baada ya kukabidhi msaada. Toka kulia ni Afisa wa Kanda ya Temeke, Lindi na Mtwara wa PPF Bi. Linda Njoolay, Meneja Uhusiano wa PPF Bi. Sarah Kibonde Msika, Meneja wa kanda ya Temeke, Lindi na Mtwara Bi.Lulu Mengele, Mganga .Mkuu wa wilaya ya Temeke Dk. Asha Mahita, Bi. Mary Msofe(watatu kushoto) Afisa uhusiano wa PPF na wafanyakazi wa hospitali ya wilaya
0 comments:
Post a Comment