Mgombea urais wa Ujerumani kutoka muungano wa chama tawala Christian Wulff kulia akiwa na Kansela Angela Merkel
Muungano unaoongoza serikali nchini
Ujerumani, wa mrengo wa kati kulia, wa Kansela Angela Merkel umemteua
waziri mkuu wa jimbo la Lower Saxony Christian Wulff kuwa mgombea wa
kiti cha urais.
Akitangaza uamuzi huo, Kansela Merkel amesema Wulff mwenye umri
wa miaka 50 ni mtu mbunifu, ambaye anaweza kuisaidia nchi kimawazo.
Vyama vya upinzani vya SPD na kile cha kijani vimemchagua
mwanaharakati wa iliyokuwa Ujerumani mashariki Joachim Gauck kuwa
mgombea wake.
Hata hivyo mgombea kutoka katika muungano wa bibi Merkel, Christian
Wulff anaelekea kushinda nafasi hiyo, kutokana na muungano huo, kuwa na
wabunge wengi katika baraza la wawakilishi ambalo ndio linachagua Rais.
Ujerumani inahitaji Rais mpya kushika nafasi ya Horst Köhler, ambaye
alijiuzulu bila ya kutegemewa mwanzoni mwa wiki.
Mwandishi:Halima Nyanza
0 comments:
Post a Comment