Zaidi ya watu miamoja wamefariki
katika ajali ya moto nchini Bangladesh, ulioteketeza majengo kadhaa
katika eneo moja lenye watu wengi zaidi mjini Dhaka.
Zaidi ya wengine miamoja walijeruhiwa wengi
wakipata majeraha mabaya zaidi.
Majengo kadhaa yaliteketezwa na moto huo
uliosambaa zaidi kwa sababu ya kemikali zilizokuwa kwenye maduka ya
karibu.
Moto huo ulisambaa katika majengo ya ghorofa na
kuwanasa mamia ya wakaazi wa majengo hayo katika eneo moja la mji lenye
idadi kubwa ya watu.
Mamlaka katika eneo hilo yamesema miili ipatayo
themanini na tano imepatikana, kiini cha Moto huo ikisemekana kuwa
mlipuko wa transformer.
BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment