SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 29, 2010

YALIOJIRI JANA EXTRA BONGO PALE NEW MSASANI CLUB.

Ali Choki aliingia na staili ya aina yake ndani ya ukumbi wa Msasani Club jana usiku tayari kwa utambulisho wa Bendi yake ya Extra Bongo. Baadae staili hiyo ilikuja kujulikana kama Igwee...! Choki haishi Vituko, Ni Burudaanii...tu.
Hao unaowaona hapo juu ni Kiumbe Group waliporomosha burudani safiiiiiiiiiiiiiiiiiii sana wakiwa kama vijana ambao wanatoka na waliweza kujitaidi kwenye steji kwa kupanda na madansa wao. Hawa jamaa wanatisha kuanzia Video Production, Audio, Dansa, Artist.
Mtu mzima Prof Jay aka Dad wa mziki huu wa Bongo fleva alikamua show ya kimataifa na alichonifurahisha kwenye wimbo wa Zali la Mentali aliitwa msichana na kuimba nae, baada ya kuwa anatunzwa wekundu kibao na Dola nyingi kutoka kwa wadau jamaa zile ela alizokuwa ameshika baada ya wimbo huo alimpatia yule binti na kumwambia asante.
Umetishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa brazaaaaaaaaaa
Wadau hawa walikuwepo pia na kuiwakilisha Kijitonyama vizuri.
Watoto wa Maimatha Jese
DJ Steve B pamoja na Joh Makini
Madansa wa Matonya wakijiandaa na show
Watoto wa Kiumbe
Hussen Machozi aliyesimama katikati akiwa full kwa show
Watu wazima wakita happy kabisa, yaani hakuna utata wala vitaaaaaaa
Dad akiwa ametupia suti safiiiiiiiiiiiiiiii kabisaaaaaaa
MC wa shughuli hiyo alikuwa Maimatha wa Jese kutoka TBC1.
Hussen Machozi akiporomosha masongi yake makali makali
Haruna akiwa amesimamia mitambo na kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa
Matonya na DJ Choka, hapa aliniambia kuwa anawaomba mashabiki wake kwamba huo uzushi unaoendelea mtaani kama amenyongwa sijui amekamatwa hao watu wanaosema waache mara moja
Dada langu la nguvu Mboni Masimba akiwa na rafiki yake na walikuwa wamependeza sana natamani kama wangesimama muwaone.

0 comments:

Post a Comment