SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 15, 2010

Mpya kutoka kwa msanii Hard Mad

Ukizungumza Hard Mad si jina geni sana katika masikio ya wadau wa Muziki huu wa kizazi kipya.
Msanii wa miondoko ya Reggae,Dancehall na pia Afro beat.Alitesa sana na ngoma kama vile "Ni Wewe" na nyingine nyinginezo.Nilipata nafasi ya kuzungumza naye na akanieleza kwamba yupo kimya kwa muda mrefu.
Katika kufanya maandalizi ya ujio wake mpya katika  kujipanga ili kuhakikisha kuwa akitoka mashabiki wake wanapata kile ambacho kimekusudiwa. Alitanabaisha 24 Seven 365 kuwa "man unajua mziki sasa umekuwa mgumu hivyo unahitaji mtu kujipanga ili ukichomomka unatoka ile ile " akimaanisha unatoka vizuri.Mashabiki wangu wakae mkao wa kula nimejiandaa vizuri na wategemee vitu vya uhakika,nategemea kuachia video mpya wiki ijayo itakuwa hewani,ngoma inaitwa "Mkali Ninae Mfahamu" (aka Ujio Mpya). Na pia kuna ngoma nyingine ambayo nategemea kuiachia soon Audio inakwenda kwa jina la "Imebaki Story". Hivyo mashabiki wake mkae mkao wa kula kwa ngoma kali zilizoenda shule, kila la heri man maandalizi mema.
Imetayarishwa na  Ally Shaaban Mgido's.

0 comments:

Post a Comment