SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 15, 2010

Kifo cha mwanaharakati wa upinzani chaongeza wasiwasi Burundi


Sample ImageMaafisa usalama nchini Burundi jana Ijumaa walitumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga mauaji ya mwanaharakati wa upinzani. Hayo yanajiri huku homa ya kisiasa ikizidi kuongezeka nchini humo kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kuanza wiki ijayo. Msemaji wa polisi ya Burundi Pierre Ntarabaganyi amethibitisha kwamba, mwanaharakati huyo aliyekuwa mwanachama wa chama cha MSD alipigwa risasi na kuuawa na kwamba uchunguzi unafanyika kuhusu suala hilo. Mtu mmoja aliyekuwa anaishi jirani na mwanaharakati huyo alisema kwamba, Eddy Munerezo aliyekuwa na miaka 27 aliuawa na watu wawili waliokuwa na sialaha wakati alipokuwa akirejea nyumbani kwake baada ya kufanya kampeni za chama hicho katika mji mkuu Bujumbura. Jumuiya ya kutetea haki za binadamu ya kimataifa imesema kwamba machafuko ya kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu wa Burundi unaoanza wiki ijayo yanahatarisha jitihada za kuimarisha demokrasia ya vyama vingi baada ya miaka kadhaa vita vya ndani nchini humo.


0 comments:

Post a Comment