SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 25, 2010

Mkutano wa vyombo vya habari vya Asia wa mwaka 2010 wafunguliwa Beijing

Mkutano mkuu wa vyombo vya habari vya Asia wa mwaka 2010 umefunguliwa tarehe 25 asubuhi hapa Beijing, wanasiasa, wasomi na wasimamizi waandamizi wapatao 800 wa vyombo vya habari kutoka Asia, Afrika, Ulaya na Marekani wamehudhuria mkutano huo.
Waziri wa propaganda wa kamati kuu ya chama cha kikomunisiti cha China Bw. Liu Yunshan, mkurugenzi wa idara kuu ya redio, filamu na televisheni ya China Bw. Wang Taihua na naibu katibu mkuu w Umoja wa Mataifa Bw. Kiyotaka Akasaka na mwenyekiti wa shirika la maendeleo ya matangazo ya Asia-Pasifiki Bw. Thoyyib Waheed wamehudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo na kutoa hotuba.
Mkutano huo ni mkutano mkubwa wa vyombo vya habari vya kimataifa ulioanzishwa na kuandaliwa na shirika la maendeleo ya matangazo ya Asia na Pasifiki. Mkutano huo ni wa awamu ya 7 na kaulimbiu yake ni 'uvumbuzi, uaminifu, haki na majukumu'.
Swahili.cri.cn/

0 comments:

Post a Comment