SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 26, 2010

Dar es Salaam-Jumuiya ya Afrika Mashariki yateketeza silaha nyepesi nchini Tanzania

Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 25 ilitekeleza silaha nyepesi 2600 mkoani Kagela, Tanzania, ili kuadhimisha siku ya ukombozi wa Afrika na shughuli za "mwaka wa amani na usalama wa Afrika" za mwaka 2010.
Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoundwa na Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi ilitoa taarifa ikisema, nchi wanachama wa jumuiya hiyo inateketeza silaha nyepesi hadharani ili kuhakikisha usalama, utulivu na mshikamano wa kisiasa kwenye sehemu ya Afrika Mashariki.
Habari zinasema kwa ujumla jumuiya hiyo imetekeleza silaha nyepesi elfu 12 na baruti tani 5. Shughuli za kuteketeza silaha nyepesi pia zilifanyika huko Bujumbura, Burundi mwezi Aprili mwaka huu.
BBC Swahili.

0 comments:

Post a Comment