SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.
Showing posts with label Kampuni ya Mawasiliano ya Etisalat Yashinda Tuzo 3 za Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Kampuni ya Mawasiliano ya Etisalat Yashinda Tuzo 3 za Kimataifa. Show all posts

Thursday, March 1, 2012

Kampuni ya Mawasiliano ya Etisalat Yashinda Tuzo 3 za Kimataifa

Huduma yake ya Mobile Baby yanyakuwa tuzo 2 wakati huduma yake ya malipo kwa kutumia simu yapewa tuzo ya ubunifu
****
Dar es Salaam, Jumatano Februari 29, 2012: Kampuni ya mawasiliano inayoongoza Mashariki ya Kati, bara la Afrika na Asia imefanikiwa kuonyesha umahiri wake kwenye sekta ya mawasiliano kwa kunyakuwa tuzo 3 kwenye kongamano la mawasiliano linalofanyika kila mwaka Barcelona, Uhispania. Tuzo mbili ni za huduma yake ya ‘Mobile Baby’ ambayo inatoa huduma za afya kwa njia ya simu na tuzo ya tatu ni kwa ajili ya huduma bunifu ya kufanya malipo ya kiasi chochote kwa njia ya simu wakitumia teknologia mpya ijulikanayo kama Near Field Communications (NFC).