Watuhumiwa wa mtandao wa ugaidi nchini wakiwa chini ya ulinzi katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana walipofikishwa
kusomewa mashtaka.
Baadhi
ya watuhumiwa wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakisindikizwa na askari wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia (FFU), kuingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam Julai 17,2014 kusomewa mashitaka yao.
Watuhumiwa wakiingia ndani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Watuhumiwa wakipelekwa maabusu baada yakusomewa mashitaka yao.Picha na Philemon Solomon na Salim Shao
---
Na Mwene Said
WAKAZI
wa jijini Dar es Salaam 16 leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na kesi mbili tofauti ikiwemo ikiwemo kula
njama na kusaidia wenzao kufanya ugaidi sehemu mbalimbali Tanzania na
kutumia mtandao wa Fesibuku kupata mbinu za kutengeza mabomu ya kwenda
kufanya ugaidi nchini Kenya.
Katika
kesi ya kwanza washtakiwa hao ni, Nassor Abdallah, Hassan Suleimani,
Anthari Ahmed, Mohamed Yusuph, Abdallah Hassan maarufu kama Jibaba,
Hussein Ally, Juma Juma, Said Ally, Hamis Salum, Said Salum, Abubakar
Mngodo, Salum Salum, Salum Amour, Alawi Amir, Rashid Nyange ama Mapala
na Amir Juma.
Mashtaka
hayo yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa wa mahakama
hiyo. Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi,
Prosper Mwangamila akisaidiana na Mawakili wa Serikali, George Barasa,
Mwanaamina Kombakono na Brenda Nick.
Barasa
alidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2013 na mwaka huu
sehemu mbalimbali nchini Tanzania, washtakiwa walikula njama ya kutenda
kosa la kusaidia kufanyika ugaidi. Ilidaiwa katika shitaka la pili, kati
ya Januari mwaka 2013 na June mwaka huu sehemu mbalimbali Tanzania,
washtakiwa wote kwa pamoja waliwasaidia Sadick Absaloum na Farah Omary
kufanya ugaidi kinyume cha sheria.
Hakimu
Riwa alisema kesi hiyo itatajwa Julai 23, mwaka huu na washtakiwa
wataendelea kukaa mahabusu. Katika kesi ya pili, mshtakiwa ni, Jihad
Swalehe anakabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo kula njama na kufanya
mawasiliano kupitia mtandao wa kijamii Facebook ya kupata mbinu za
kufanya ugaidi nchini Kenya. Nick alidai kuwa siku na mahali
pasipofahamika jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikuwa na njama ya
kutenda kosa la kigaidi.
0 comments:
Post a Comment