Kikosi
cha Taifa Stars kimerejea jijini Dar es Salaam leo kutoka Mbeya ambapo
Jumapili (Julai 20 mwaka huu) kitapambana na Msumbiji (Mambas) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Benchi
la Ufundi la Taifa Stars pamoja na wachezaji kesho (Julai 18 mwaka huu)
saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli
ya Protea Courtyard iliyopo Upanga Seaview jijini Dar es Salaam.
Naye
mchezaji Mwinyi Kazimoto amewasili leo 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar
Airways kutoka Qatar ambapo anacheza mpira wa miguu katika klabu ya Al
Markhiya ya huko. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
imepiga kambi katika hoteli ya Protea Courtyard.
=======
WAKATI HUO HUO NAO
SERENGETI BOYS MORALI JUU KUWASUBIRI AFRIKA YA KUSINI
Kocha
Mkuu wa Serengeti Boys, Hababuu Ali Omari amesema morali ya wachezaji
wake ipo juu kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos)
itakayochezwa kesho (Julai 18 mwaka huu).
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 17 itafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo
Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF jijini Dar es
Salaam leo, Kocha Hababuu amesema nia ya kikosi chake ni kuhakikisha
wanafika kwenye fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Niger.
“Tunaiheshimu
Afrika Kusini, lakini hatuiogopi. Morali ya wachezaji ipo juu na
wanajiamini. Kimsingi wanajua kuwa hii ndiyo njia ya wao kutokea kwenye
mpira wa miguu, kwa hiyo lengo ni kushinda,” amesema Kocha Hababuu.
Naye
Kocha wa Afrika Kusini, Molefi Ntseki amesema anaziheshimu timu za
Tanzania, na changamoto aliyonayo ni kuhakikisha kuwa anashinda mechi
hiyo kwani mara ya mwisho kwa timu yake kushiriki fainali za Afrika
ilikuwa miaka sita iliyopita.
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000 na tiketi zitapatikana uwanjani kwenye magari maalumu.
0 comments:
Post a Comment