Ni
mchezo wa hatari na unaotia woga kama hujawahi kuendesha Pikipiki
unapoona wakikimbizana na kupitana katika kona kali na kuruka matuta
huku wakionyesha mbwembwe kibao wakiwa kwenye mwendo mkali.
Lakini pia
ni mchezo mzuri na unaovutia hata ukiwa ni mara yako ya kwanza
kuushuhudia kwa hakika utavutiwa na kuulizia ratiba za mchezo huu ili
uweze kujipanga na ratiba zako uweze kuwa wakifika kwenye Viwanja wa
Tanganyika Parkers Kawe jijini Dar es Salaam, kujionea mwenyewe bila
kiingilio usisubiri kuadithiwa.
Aidha
ni miongoni mwa michezo inayopendwa zaidi duniani ukiondoa Soka, lakini
kwa hapa kwetu nchini Tanzania bado mchezo huu unaonekana kutelekezwa
na kutopewa kipaumbele na wadau na wahusika wa michezo na hata viongozi
kiasi cha kuufanya mchezo huu kubaki kuwa ni wa kujifurahisha tu tena
wenyewe kwa wenyewe tena katika eneo lisilo rasmi kwa mchezo huu pale
maeneo ya Kawe, baada ya wachezaji wenyewe kujichagulia eneo hilo na
kuanza kufanya mazoezi yaliyowavutia baadhi ya watu ambao wameonekana
kuupenda na kujikuta kila siku ya jumapili wakifika Kawe kushuhudia.
Kwa
hakika hata wadhamini pia wameonekana kutoutilia maanani mchezo huu, na
wengi wakionekana kuwekeza zaidi kwenye mchezo wa Soka na mingineyo,
huku vipi?????.
Kiukweli
wadau tumeutupa sana mchezo huu ambao kiuhakika unaweza kutuletea hata
medali nyingi tu kimataifa kutokana na wachezaji wengi wazuri
wanaojitolea kwenda kushiriki mashindano ya kimataifa kimya kimya na
kufanya vizuri, ambapo pia wengi wao hawajaweza kutoka nje ya Afrika
Mashariki. Wazir wa Michezo Tafadhali mchezo huu tunaomba uuangalie kwa
jicho la pili na ikiwezekana ukutane na wachezaji hawa ili kuzungumza
nao ikibidi kuwasaidia kupata wadhamini na kuwatengenezea uwanja ili
waweze kuwaalika hata wenzao ambao wamekuwa wakiwaalika kimataifa.
Wachezaji hao wakiwa katika mazoezi Jumapili iliyopita.
Wakiruka matuta.......
Mashindano ya wenyewe kwa wenyewe yakiendelea....
Wapo wazuri zaidi ha hawa pia......
0 comments:
Post a Comment