Kiongozi
wa mwenge kitaifa mwaka 2014,Rachel Kassanda akiwataka wananchi wa
kilwa kujiunga na CHF,kwani ndiyo mkombozi wa matibabu sasa kwa
kuzingatia maboresho ya huduma za afya yanavyowezekana chini ya sera ya
urasimishaji wa majukumu kwa jamii hususani ya uchangiaji baina ya
wananchi na serikali,ambapo mfuko wa taifa wa bima ya afya unasimamia
mfuko wa afya ya jamii kwa niaba ya serikali ,kulia ni mkuu wa wilaya ya
Kilwa mhe.Abdalla Ulega ambaye ndiye mwenyeji wa mapokezi ya mwenge wa
uhuru.
Meneja
wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi,Fortunata Kullaya
akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la upimaji afya na mwitikio wa
wananchi wa kilwa ambapo takribani wananchi 257 walijitokeza kupimwa
afya na kaya 73 zilijiunga papo kwa papo na CHF Kwenye banda la mfuko
kwa kiongozi wa mwenge kitaifa kwa mwaka 2014 Rachel Kassanda,ambaye
alikagua shughuli mbalimbali zilizokuwa zikitekelezwa kwenye viwanja vya
shule ya msingi somanga ambapo mwenge wa uhuru ulipokelewa,kulia ni
mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe. Abdallah Ulega.
Mkazi
wa kata ya somanga Fatuma Likondwe akipata huduma ya upimaji wa
shinikizo la damu kutoka kwa daktari Salama Bimbire,zaidi ya watu 257
waliweza kupatiwa huduma za vipimo kwa magonjwa yasiyoambukiza na
wastani wa asilimia 58% ya waliopimwa walikutwa na shinikizo la damu
(BP) na hawakujitambua hapo kabla.
Wananchi
wa Kilwa wakiwa kwenye foleni ya kupata huduma za vipimo kwenye banda
la Mfuko wa taifa wa bima ya afya ambapo huduma za upimajiwa kiwango cha
sukari kwenye damu (RBG),shinikizo la damu (BP),uwiano wa uzito na
urefu wa mwili (BMI) na ushauri wa kitaalamu ulitolewa na
madaktari,wakati wa mapokezi ya mwenge wa uhuru kwenye viwanja vya shule
ya msingi Somanga-Kilwa.
Picha na Paul Marenga-NHIF LINDI
0 comments:
Post a Comment