JESHI
la Polisi jijini Arusha limewakamata watu 16 akiwemo Imam wa Msikiti wa
Al Quba uliopo mkoani Arusha, Jafar Lema na mfanyabiashara 1 wote
wakihusishwa na matukio ya ulipuaji wa mabomu jijini Arusha.
Polisi Arusha limekamata mabomu 7 na risasi 6 na unga wa baruti.
Jeshi la polisi mkoani Arusha limekamata mabomu saba ya kurushwa kwa mkono risasi sita za shootgun na unga wa baruti vikiwa vimefichwa kwenye nyumba moja iliyoko kata ya Sombetini jijini Arusha na jumla ya watu 25 wanashikiliwa.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai
nchini (DCI), Issaya Mungulu, katika mkutano wake na waandishi wa habari
jijini Arusha leo, Jumanne Julai 22, 2014 imedaiwa kuwa Julai 21, 2014
saa 20.00 usiku katika maeneo ya Sombetini, Jeshi hilo limewakamata
Yusufu Ally (30) na mkewe Sumaiya Juma (19) wakiwa nyumbani kwao baada
ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono Saba (7), risasi
sita za bunduki aina ya shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja.
Mungulu amenukuliwa na mtandao wa FikraPevu akisema
kuwa Yusufu ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa
ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha na kuwa mahojiano juu ya
mtuhumiwa bado yanaendelea dhidi yake.
Aidha,
amesema uchunguzi wa shauri hilo pamoja na matukio mengine ya milipuko
yanaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa
polisi na kuwakamata watakaobainika kuhusika na matukio hayo.
Mtuhumiwa mwingine wa milipuko nchini asakwa na Polisi
Hata
hivyo, Jeshi hilo limesema linamtafuta, Yahya Hella (33) mkazi wa
Mianzini mkoani humo, mwenyeji wa Chemchemu, Kondoa – Dodoma kwa tuhuma
za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini.
“Zawadi
nono itatolewa kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazowezesha
ukamatwaji wa mhalifu huyu na pia nipende kuwashukuru sana wananchi kwa
ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa jeshi letu hapa nchini” alisema
Mungulu.
Watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani
Amesema
kufuatia tukio la mlipuko wa bomu Julai 7, 2014 saa 22.15 usiku katika
mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha, ambapo watu wanane
walijeruhiwa vibaya, Jeshi hilo limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi
na kuwa kati yao watu sita watafikishwa Mahakamani mapema iwezakanavyo.
Amewataja
watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo kuwa ni pamoja na
Shaaban Mmasa (26) ambaye ni mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye
mgahawa huo, Athuman Mmasa (38) na Mohamed Nuru (30), wote walinzi
katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la Gymkhana jirani na eneo la
tukio.
Wengine
ni Sheikh Jaffar Lema (38) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi
Olturmet katika wilaya ya Arumeru, pia alikuwa Imam wa Msikiti wa
AL-QUBA mjini Arusha ambaye ametambuliwa kama mmoja wa viongozi
walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo balimbali nchini, Abdul
Salim (31), wakala wa Mabasi Stendi Arusha, na Said Temba
(42), mfanyabiashara wa Arusha.
Kwa mujibu wa Mtandao wa JamiiForums,
inadaiwa kuwa kuna vijana wamekuwa wakisafirishwa kwenda Somalia
kujifunza ugaidi na Alshabab lakini wananchi wanalilalamikia Jeshi la
Polisi kwa kutochukua hatua mapema.
SOURCE: Fikra Pevu
0 comments:
Post a Comment