Afisa
Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias
akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana wasikilizaji juu ya
masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi
kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya kuwajengea
uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa ufuatiliaji wa
vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika
kwenye kituo cha Redio Nuru FM mjini Iringa.
(Picha zote na Zainul
Mzige).
Na Mwandishi wetu
Tafiti
zimebaini kwamba Vijana hawatumii Kondomu na hutoa sababu nyingi ikiwa
ni pamoja na kutopata ladha wakati wa tendo la ndoa na kwamba inapunguza
nguvu na visingizio vingine vingi vinavyopelekea kuashiria hatari ya
maambukizi.
Hayo
yameelezwa na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO,
Bw. Herman Mathias wakati akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana
wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya
VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika
warsha ya kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa
ufuatiliaji wa vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA
Redio.
“Asilimia 40 ya Wasichana na Asilimia 47 ya Wavulana ndio wenye ufahamu
wa kina juu ya maambukizi ya VVU huku asilimia kubwa wakiwa hawana
elimu ya kutosha na hawajui afya zao kwa kuwa hawana utamaduni wa kupima
VVU ”, amesema Bw. Mathias.
Mkufunzi
wa warsha hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah
Mfuruki akiwapiga msasa washauri wa Vikundi vya Vijana kwenye warsha ya
siku mbili inayoendelea mjini Iringa.
Katika
warsha hiyo ya siku mbili inayoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na
UNICEF katika kituo cha Redio cha Nuru FM Iringa, Bw. Mathias amesema
kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu sahihi kwa Vijana ya kujikinga na
maambukizi ya VVU na Mimba kutokana na uelewa mdogo wa Vijana katika
matumizi sahihi ya Kondomu.
Wakichangia
mada kuhusu masuala muhimu yanayowahusu vijana katika maambukizi ya VVU
vijana wamesikitishwa na mimba za utotoni kwa wasichana zinazochangia
vifo vya Mama na Watoto na wasichana kuacha masomo.
Washiriki
wa warsha hiyo wametaka hatua za haraka zichukuliwe kuhakikisha kuwa
sheria za mtoto zinazoruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo
zinafanyiwa marekebisho ya haraka kulinda haki ya mtoto wa kike.
Mmoja wa washiriki akihoji jambo kwa mkufunzi wakati wa mafunzo hayo.
Wakijadili
mada hiyo washiriki wamesema mila na tamaduni pia zinachangia kwa kiasi
kikubwa kumkandamiza mtoto wa kike katika masuala mbalimbali ya
maendeleo yake.
Wakitoa
mifano ya baadhi ya mila zilizowafanya wapaze sauti kuhusu mabadiliko
ya sheria za mtoto ni ile sheria ya ndoa na mila inayoruhusu mtoto wa
kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kwa ridhaa ya wazazi. Umri huo
unakinzana na haki za mtoto kufurahia maisha yake na kupata elimu.
Mifano mingine ya kitamaduni ni pale mwanamume anapochumbia mimba wakati akijua wazi mtoto ana haki zake za msingi za kuishi.
Wamezitaja
pia asasi za dini kutoa elimu kwa vijana ili kusaidia hali
iliyojitokeza ya wazazi kutokuwa na muda na watoto wao kuwaelimisha
kuhusu mabadiliko ya miili na afya zao.
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akifafanua jambo kwa washiriki.
Akitoa
mada kuhusu mbinu mbalimbali za kuwezesha majadiliano katika vikundi
vya wasikilizaji, Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdul
Mfuruki amewataka wawezeshaji kutotumia nafasi walizonazo ili kuendesha
mjadala wenye tija.
Amesema
washauri wa vikundi hawana budi kuweka mizania kutumia busara, kusoma
mazingira na kutoingiza imani au itikadi itakayopelekea kuharibu mjadala
unaoendeshwa wa kufuatilia vipindi vya SHUGA Redio, kuwa wavumilivu,
kusoma na kuheshimu mawazo ya wengine na kutofungamana na upande wowote
ili kumweleza mshiriki wa majadiliano kufunguka zaidi.
Bw.
Mfuruki amesema vijana wa vikundi vya wasikilizaji kuwaza mambo mengi
ni vyema kuwasikiliza kwa uvumilivu, kupata ushauri wa wengi kwa lengo
la kufanya maamuzi sahihi bila kulazimishana na vile vile kuwa wabunifu
kwa kutumia mbinu mbadala ili kupata habari iliyojificha.
Mkufunzi
Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah Mfuruki akiwaelekeza
jambo washiriki wakati wa mazoezi ya vikundi kazi kwenye warsha hiyo.
Pichani juu na chini ni baadhi washauri wa vikundi vya vijana
wakifuatilia kwa umakini warsha hiyo kwa ajili ya kutekeleza Mradi mpya
wa SHUGA Redio wenye lengo la kuendeleza kampeni za hamasa kwa vijana
kupunguza maambukizi mapya ya VVU kupitia Redio za Jamii nchini.
Pichani juu na chini ni Washiriki wakijidiliana kwenye vikundi kazi wakati wa warsha hiyo.
Mkufunzi
wa warsha hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah
Mfuruki akitoa mwongozo wa kazi za vikundi kwa staili ya aina yake kwa
washiriki wa warsha ya siku mbili katika utekelezaji wa Mradi mpya wa
SHUGA Redio.
Pichani
juu na chini washiriki akitolea maelezo ya picha aliyoichora
ikimaanisha nini wakati wa warsha hiyo ya siku mbili inayoendelea mjini
Iringa.
0 comments:
Post a Comment