Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam jana, Katibu mkuu wa Yanga, Beno Njovu alisema uamuzi wa kuvunja
Kamati ya Utendaji na kuteua wajumbe wapya ni kwa mujibu wa azimio namba nne la
mkutano wa wanachama kuhusiana na mabadiliko ya katiba yaliyofanyika Januari 20,
2013. Njovu alisema katika
mkutano huo, wanachama wa Yanga walimpa mamlaka mwenyekiti na makamu wake
kuvunja au kuteua wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kamati nyingine za klabu
hiyo.
Alisema wajumbe wa
sasa wa Kamati ya Utendaji watamaliza muda wao Julai 31 na wapya wataanza kazi
Agosti Mosi. “Uamuzi
huu ni kwa mujibu wa Ibara ya 28 kifungu kidogo cha kwanza cha katiba ya klabu.
Hivyo ni uamuzi sahihi ambao mwenyekiti na kamati yake wameupitisha.
Tunawashukuru wajumbe waliotumikia klabu hiyo kwani bado ni wanachama wetu,”
alisema Njovu. Wajumbe
wapya walioteuliwa na Manji na Sanga ni Abubakari Rajabu, ambaye amepewa kazi
ya kusimamia mradi wa Jangwani City, Sam Mapande (sheria na utawala bora),
George Fumbuka (uundwaji wa shirika), Wazir Barnabas (vibali vya hatimiliki na
mahusiano na wafadhili) na Abbas Tarimba, ambaye atashughulikia mipango na
uratibu.
Wengine
katika orodha ya wajumbe wapya ni Isaac Chanji na Seif ‘Magari’ Ahmed
(uendeshaji wa michezo), Musa Katabalo (mauzo ya bidhaa), Mohamed Bhinda (ustawishaji
matawi), David Sekione (uongezaji wa wanachama) na Mohamed Nyenge, ambaye
atashughulikia masuala ya utangazaji wa habari, taarifa na matangazo. Njovu
alifafanua kuwa wajumbe wa kamati hiyo mpya pia watakuwa na kazi ya kusimamia
kamati ndogo ndogo za klabu hiyo. Alisema Mapande atasimamia Kamati ya Maadili,
Nidhamu na Uchaguzi wakati Fumbuka na Barnabas watasimamia Kamati ya Uchumi na
Fedha, huku Seif Magari na Isaac Chanji wakisimamia Kamati ya Mashindano, Soka
la Vijana na Wanawake na Ufundi. Akizungumzia kutoswa
kwake katika Kamati ya Utendaji ya Yanga, Bin Kleb alisema miezi miwili
iliyopita aliwaomba viongozi wasimteue kwenye Kamati ya Utendaji.
Habari kwa hisani ya http://www.mwananchi.co.tz/
0 comments:
Post a Comment