Meneja wa Arsenal,Arsene Wengerameonekana kukiri kumhusudu zaidi nyota wa Juventus,Arturo Vidal.
Mfaransa huyo anataka kuishinda klabu ya Manchester United kwa kupeleka ofa ya pauni milioni 44 kwaajili ya kupata huduma ya raia huyo wa Chile.
Wenger anataka kuimarisha kikosi chake kwaajili ya msimu ujao kufuatia kushindwa kufikia malengo ya kutwaa taji la ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita.
Klabu hiyo ya Emirates pia imeungana na Bayern Munich,Roma na Paris Saint-Germain katika kumshawishi beki wa kulia wa Newcastle,Mathieu Debuchy ambaye yupo na Ufaransa kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Liverpool hawatomruhusu Luis Suarez kuondoka klabuni hapo majira haya ya joto kwa kiasi cha pungufu ya pauni milioni 80.
Barcelona na Real Madrid wanaendelea kumuwania raia huyo wa Uruguay ambaye amepata adhabu ya kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi minne na Fifa.
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund,Pierre-Emerick Aubameyang yupo katika mazungumzo ya mwisho na klabu ya Chelsea juu ya uhamisho wa kwenda Stamford Bridge.
Arsenal na Tottenham wanaandaa ofa ya mwisho kwa mshambuliaji wa Real Madrid,Alvaro Morata wakati Juventus wameweka mezani kiasi cha Euro milioni 20 ili kumnasa mhispania huyo.
Liverpool wapo katika mikakati ya kumsajili chipukizi wa Ubelgiji,Divock Origi kutoka klabu ya Lille huku wakiwa na mipango ya kumrudisha mchezaji huyo kwa mkopo katika klabu hiyo ya Ufaransa endapo watafanikiwa kumpata.
Pia klabu hiyo ya Anfield inajiandaa kupeleka ofa kwa winga wa Benfica,Lazar Markovic ambaye mkataba wake unathamani ya kiasi cha pauni milioni 25.
Manchester United wamezidi kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Juventu,Arturo Vidal na wapo katika mazungumzo na mabingwa hao wa Seria A juu ya kutaka kupata saini ya raia huyo wa Chile.
Beki wa kati wa Mexico na Espanyol,Hector Moreno yupo katika orodha ya wachezaji wanaohitajika na meneja wa Marseille,Marcelo Bielsa huku akitazamia kumsainisha kwenye timu hiyo ya Ligue 1.
Klabu hiyo ya Ufaransa inaonekana ipo makini sana juu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye alikiri kutovutiwa na klabu za Tottenham Hotspur and Hull City.
Klabu ya Tottenham kutoka mitaa ya London inakaribia kukamilisha mpango wa kumsajili kiungo wa kiargentina,Esteban Cambiasso kutoka Inter Milan.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 atapatikana kwa uhamisho huru wakati mkataba wake na klabu ya Seria A utapomalizika mwishoni mwa mwezi huu(Juni).