
Binti Farida Abdalah (18) ambaye ni mlemavu wa viungo na akili akiwa
amekaa kwenye kochi nyumbani kabla ya kupelekwa Ofisi za Dawati la
Jinsia la Polisi. Picha na Hamida Shariff, Mwananchi
------
Wazazi wa binti mwenye ulemavu wa viungo na akili, Farida
Abdalah (18) mkazi wa Lukobe Juu wameiomba Serikali, wasamaria wema na
wadau mbalimbali kumsaidia binti yao huyo ambaye kwa sasa amelazwa
katika hospitali ya rufaa na anaendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya
yake.
Pia wazazi hao ambao walionekana kuwa na hali
ngumu ya kimaisha waliomba msaada wa kupatiwa matibabu ya viungo na
akili kwa binti yao ili aweze kutembea na kujitambua, kwani kwa sasa
binti huyo amekuwa akilala tu kitandani.
Maisha ya binti huyo ambaye umri wake haulingani
na umbo lake yameguswa na watu wengi, kwani amekuwa haongei, halii,
hasikii na wala hajitambui hivyo amekuwa akivalishwa nepi na kubebwa
kama mtoto mchanga.
Akitoa historia ya binti huyo kwa mwandishi wa
habari hizi jana mama mzazi wa binti huyo Mwajuma Abdalah alisema kuwa
Farida alizaliwa mwaka 1996 wilayani Muheza mkoani Tanga na
alijifungulia nyumbani.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea........