Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dkt. Joseph Komwihangiro,
Mkurugenzi wa Marie Stopes kwa kuwa mstari wa mbele katika huduma na
elimu za mzazi wa mpango Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua huduma
za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti
Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.Wengine toka
kushoto ni Mama Salma Kikwete, Mlezi wa MEWATA, Dkt. Serafina Mkuwa,
Mwenyekiti wa MEWATA, Mhe. Kebwe Steven Kebwe (Mb.), Naibu Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, kulia kabisa ni Mbunge wa Tabora Mjini Mhe.
Ismail Aden Ragge.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea Jumamosi Mei 7, 2014 wakati
akizindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na
saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani
humo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanakwaya wa kambi ya Msange
JKT ya Tabora Jumamosi Mei 7, 2014 baada ya kuzindua huduma za
uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani
Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Tabora Mjini Mhe Ismail
Aden Ragge Jumamosi Mei 7, 2014 baada ya kuzindua huduma za
uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani
Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.PICHA NA IKULU
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameamuru Jeshi
la Polisi kupeleleza na kisha kuwachukulia hatua mara moja watu wote
wanaotuhumiwa kwa wizi na ubadhilifu katika vyama vya ushirika mkoani
Tabora.
Rais Kikwete amesikitishwa sana na tuhuma hizo zilizosababisha
kuwepo kwa tatizo la muda mrefu kwa wakulima wa tumbaku kwa kutokulipwa
stahili zao na vyama vya ushirika kwa muda mrefu.
Alisema:
"Kwa upande wa tatizo la wakulima wa tumbaku kutokulipwa stahili zao na
vyama vya ushirika nimeelezwa na kulielewa. Kuna tuhuma za wizi na
ubadhilifu.
“Nimemuagiza
Inspekta Jenerali wa Polisi atume watu wake wa upelelezi wa makosa ya
Jinai waje wafanye uchunguzi ili wahusika wakamatwe na kufikishwa
Mahakamani na kupewa adhabu zinazostahili.
“Ameniahidi
kuwa keshokutwa (Jumatatu) watu hao watakuja. Wapeni ushirikiano
unaostahili ili tukomeshe uhalifu na dhuluma zinazofanywa na Maofisa wa
Vyama vya Ushirika na taasisi za fedha kwa muda mrefu sasa".
Rais
aliyasema hayo Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua huduma za
uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani
Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
Rais
Kikwete alisisitiza kwamba zoezi la kuchukuliwa hatua watuhumiwa wa wizi
na ubadhilifu katika vyama vya ushirika lisifanywe la kisiasa, na
kwamba asiogopwe wala kuonewa haya mtu yeyote anayehusika hata awe nani.