SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, June 19, 2014


THURSDAY, JUNE 19, 2014

SIKU YA SIKOSELI DUNIANI YAADHIMISHWA LEO


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dkt. Sarah Maongezi (aliyevaa suti ya bluu) ,akiteta jambo na  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Eligius Lyamuya ,(wapili kushoto)  mara alipomaliza kuongea na wageni waalikwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo, kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto na Mkuu wa Idara Muhimbili, Dk. Mary Charles na aliye vaa suti nyeusi ni  Mkurugenzi wa Tiba Muhimbili,  Dk. Hedinga Swai,(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)Mmiliki wa www.ujijirahaa.blogspot.com.(ukurasa wa ujijirahaa).

Sehemu ya Madaktari na aliye vaa kitambaa ni mmoja mwenye Siko Seli,ambaye anafata ushauri wa Madaktari 
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk. Sarah Maongezi,akiongea na wageni waalikwa na ndugu na jamaa leo katika Maadhimisho ya Siko Seli Duniani yaliyo fanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam.
Daktari Bingwa wa Siko Seli wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Dkt Julie Makani (kushoto) ,akiwa makini kwa kumsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dkt. Sarah Maongezi,alipkua akionge na ndugu na jamaa.
Baadhi ya watoto wanao sumbuliwa na Ugonjwa wa Siko Seli , wakiwa na wazazi wao wakimsikiliza , Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk. Sarah Maongezi

Baadhi ya watoto wanao sumbuliwa na Ugonjwa wa Siko Seli , wakiwa na wazazi wao wakimsikiliza , Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk. Sarah Maongezi
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk. Sarah Maongezi(mwenyesuti ya bluu), akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kliniki mpya ya watu waishio na seli mundu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Seli Mundu Duniani, Muhimbili Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Eligius Lyamuya na Mkurugenzi wa Tiba Muhimbili,  Dk. Hedinga Swai na kutoka kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu, Dk. Alex Magesa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto na Mkuu wa Idara Muhimbili, Dk. Mary Charles.
Picha ya pamoja na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) na wafadhili.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk. Sarah Maongezi,katika picha ya pamoja na watoto wenye Siko Seli
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk. Sarah Maongezi, katika picha ya pamoja na watoto wenye Siko Seli pamoja na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) Dar es Salaam leo katika Maadhimisho ya Siko Seli Duniani.








Waziri Membe akutana na Mabalozi wa Marekani, China, Cuba, Japan, Msumbiji na Ujerumani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkaribisha kwa furaha na kwa mara ya kwanza ofisini kwake Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Mark Childress alipofika e kwa ajili ya kujitambulishana pia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani.
Mhe. Membe na Mhe. Childress katika picha ya pamoja.
Mhe. Childress akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili Ofisini kwa Mhe. Membe
Mhe. Membe na Balozi Childress wakiwa katika mazungumzo
Mhe. Childress na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Membe na Mhe. Childress pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa China hapa nchini,  Mhe. Lu Youqing alipofika kwa ajili ya mazungumzo ambayo yalihusu pia ziara ya Makamu wa Rais wa China atakayoifanya hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 26 Juni, 2014.
Mhe. Balozi Lu akimweleza jambo Mhe. Membe wakati wa mazungumzo yao.
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Balozi LU (hawapo pichani)

 Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Cuba

Mhe. Waziri akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa Cuba hapa nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushrikiano kati ya Tanzania na Cuba. Tanzania na Cuba zinashirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na siasa.
Mhe. Membe akimsikiliza kwa makini Balozi Tormo.

Mazungumzo yakiendelea huku Afisa Mambo ya Nje, Bw. Lucas Mayenga akinukuu.

Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Japan

Mhe. Membe akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaki Okada alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.

Mhe. Balozi Okada akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Membe.

Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Nathaniel Kaaya akifuatili mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Okada (hawapo pichani)

Mkutano wa Mhe. Membe na Kaimu Balozi wa Ujerumani

Mhe. Membe akimkaribisha ofisini kwake Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Bw. Hans Koeppel alipofika kwa mazungumzo na Mhe. Waziri  kuhusu salamu za shukrani kwa Serikali ya Tanzania kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Frank-Walter Steinmeir kufuatia ziara yake ya mafanikio aliyoifanya hapa nchini mwezi Machi 2014

Mhe. Membe akipokea barua ya salamu hizo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini (hawapo pichani)

Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Msumbiji

Mhe. Membe akizungumza na Balozi wa Msumbiji hapa nchini, Mhe. Vicente M. Veloso alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Balozi Veloso na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Mhe. Membe alipozungumza nao. Picha zote na Rosemary Malale