Naibu Mkurugenzi wa kanda wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini ,Victor Nkya akizungumza wakati semina ya siku moja kwa maofisa wa polisi wa ngazi mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro.
|
Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA, Injinia Annette Matindi akizungumza wakati wa semina hizo
|
Mkuu wa kikosi cha Upelelezi mkoa wa Kilimanjaro SSP ,Ramadhan Ng'anzi akizungumza katika semina hiyo.
|
Baadhi ya washiriki katika semina hiyo ambao ni maofisa wa ngazi mbalimbali katika jeshi la polisi.
|
Baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi wakijitambulisha katika semina hiyo.
|
Kamanada wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,SACP Rober Boaz akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa TCRA,kulia kwake ni Naibu Mkurugenzi wa kanda wa TCRA,Victor Nkya na kushoto kwake ni Meneja wa TCRA kanda ya kaskazini mhandisi Annete Matindi.
|
Washiriki wa semiana wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi .
|
Baadhi ya washiriki wakibadirishana mawazo wakati wa mapumziko.
|
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
HALMASHAURI ZATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO MIRADI YA MAENDELEO
Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia PatrickMfugale akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42) unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB)uliyofanyika jijini Arusha
Mkuu wa Mkoa Arusha Magessa Mulongo akiongea katika uzinduzi huo
Kulia Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema katikati Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela na mkurugenzi wa jiji la Arusha
HALMASHAURI mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Aidha kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha miradi hiyo ikiwemo ya wananchi kukataa kulipwa fidia kwa taratibu za sheria za nchi ili kutoa maeneo ya kuchimbwa changarawe, kokoto na kuchota maji.
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale wakati akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42) unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB) uliofanyika katika ukumbi wa naura springs mjini hapa.
Alisema kuwa,kumekuwepo na changamoto kubwa sana zinazosababishwa na wananchi na baadhi za halmashauri katika utekelezaji wa miradi hiyo hali ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa katika kufikia malengo yaliyowekwa.
Alifafanua kuwa, halmashauri za wilaya pamoja na serikali za vijiji wamekuwa wakitoza kodi mbalimbali kwa vifaa vya ujenzi kama kifusi, mchanga,kokoto,na maji.
Mfugale alisema kuwa,mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha-holili ni sehemu ya mradi wa kimataifa unaojulikana kwa jina la Holili/Taveta –Voi unaounganisha nchi yetu na nchi jirani ya Kenya utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 223.
Alisema kuwa, awamu ya kwanza ni kuijenga kwa njia nne sehemu ya barabara kutoka Sakina –Tengeru (km 14.1) na Arusha bypass (km 42) kwa fedha za mkopo kutoka ADB .
Aliongeza kuwa, sehemu ya pili ni kuendeleza ujenzi wa njia nne kutoka Tengeru hadi Usa river (km 8.2) na ukarabati wa sehemu ya barabara iliyobaki hadi Holili baada ya kupata fedha.
Naye Mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), Injinia Patrick Musa alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya hali ya hewa ambayo imekuwa ikichangia mradi kukamilika kwa wakati na ucheleweshaji wa ulipwaji wa fedha za wakandarasi .
Alisema kuwa, wao kama benki ya maendeleo ya Afrika wataendelea kutafuta hela kwa ajili ya maendeleo kwani ni fursa nzuri wao kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo.(jamiiblog Pamela Mollel)