SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, June 18, 2014

NSSF YAHITIMISHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE KANDA YA ZIWA

Banda la NSSF.
Maofisa wa NSSF wakisikiiza kwa makini Hotuba ya
Mgeni Rasmi wakati wa Ufunguzi wa Kambi ya upimaji Afya Bukoba.
Meza kuu wakifurahi wakati wimbo wa mkoa wa Kagera ukiimbwa.
Toka Kushoto, Dr.Ruta Thomas, Mganga Mkuu mkoa wa Kagera, Bw.Adoh Mapunda
,Mkurugenzi wilaya ya Bukoba, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, Mkuu wa mkoa wa
Kagera, Bw.Leornard Faustine Kachebonaho, Mwenyekiti wa Chama cha msalaba
mwekundu , Kagera . Dr.Ali Mtulia Meneja wa Mafao ya Matibabu –SHIB na Mratibu
wa Chama cha Msalaba mwekundu mkoa wa Kagera, Bi.Robi Wambura.
Mkuu wa mkoa Kanali Mstaafu Fabian Massawe akisisitiza jambo
wakati wa risala yake ya ufunguzi.
Dokta Ali Mtulia, Meneja wa Mafao ya Matibabu NSSF akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, watatu toka kushoto, Huku Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dr.Ruta Thomas(wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa wilaya ya Bukoba, Bw.Adoh Mapunda(wa pili Kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Kagera , Bw.Leonard F Kachebonah0 (wan ne toka kushoto) wakisikiliza kwa Makini.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Masawe (katika), akikagua mabanda wakati wa zoezi la kupima afya bure kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.
Ofisa Uhusiano Jumanne Mbepo akimkabidhi Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe vipeperushi na Fulana alipotembelea banda la kutoa elimu kwa umma juu ya NSSF.
Wakazi wa mkoa wa Kagera wakijiandikisha kwa ajili ya kupima afya.
:D okta  Ali Mtulia akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Kagera,
Kanali Mstaafu Fabian Massawe aweze kukagua mabanda yanayotoa huduma za
upimaji.
Dokta Ali Mtulia akimuelekeza Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu, Fabia Masawe upimaji wa Uzito na
Urefu ili kutambua uwiano wa uzito na urefu kwa lengo la kushauri lishe bora.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Masawe, akiuliza maswali
na kujibiwa na Dk.Ali Mtulia kuhusu huduma zitolewazo na NSSF.


Shirika la Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF), lahitimisha 
  kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa
kanda ya Ziwa.
 
Lengo la kambi hizi zilikuwa
ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama
wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga
tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha
ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.
 
Zoezi ambalo lilianzia mkoa
wa Mara na kupata mwitiko mkubwa wa wakazi wa Mara kwa kupima watu 1582 na kufuatiwa na mkoa wa Shinyanga
hususani wilaya ya Kahama ambako walijitokeza watu 700, Mkoa wa Geita ambako watu
1000 walijitokeza, 
litahitimishwa
kwa kupima wakazi wa Mkoa Kagera wilaya ya Bukoba Mjini 
 , kwenye Viwanja vya Mashujaa (Platform),  kuanzia tarehe 14/06/2014,  kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili
asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.


HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma
mbalimbali zitatolewa  kwenye kambi hizi zikiwemo;
  Upimaji wa Shinikizo la damu
Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa
Unene)
Utoaji wa dawa za Minyoo
 Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na
Matatizo
Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
  Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji
wa Afya.
Huduma  zote hizi
zitatolewa na NSSF, BURE.
Pia kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu kwa hiyari
kwenye kambi hii ya Bukoba ambalo litaendeshwa na chama cha msalaba mwekundu.
 
NSSF inaendelea kuwasii na
kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI
Scheme. 


NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji
wadogo, Ushirika wa Bodaboda, Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa
Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.


Wananchi wa kanda ya ziwa
wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa
afya zao Bure.