Godbless
Lema Mbunge wa Arusha mjini akiwahutubia wananchi waliojitokeza kukiunga
mkono chama hicho katika viwanja vya Orofea mkoani Iringa
=====
Na Mathias Canal, Kwanza Jamii-Iringa.
Ukawa
waendelea na msimamo wa kutorejea kwenye bunge la katiba kutokana na
katiba hiyo kutokidhi matakwa ya watanzania walioshiriki kutoa maoni yao
ambayo kwa sasa yamebadilishwa na kuwa mawazo ya wachache.
Hayo
yamebainishwa na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema alipozungumza na
Kwanza Jamii ili kutaka kujua msimamo wa ukawa kurejea kwenye bunge la
katiba mapema mwanzoni mwa mwezi wa nanae.
Lema
amesema kuwa huo ni msimamo wa Ukawa unaoundwa na chama cha NCCR
Mageuzi, CUF na CHADEMA lakini pia ni msimamo wa wenyeviti wa vyama
hivyo vya ukawa.
Lema
ameongeza kuwa lengo la kuondoka bungeni ni kutokana na chama tawala
kutaka kuleta msimamo wao badala ya maoni ya wananchi kwani lengo lao
sio kutengeneza katiba yenye kurasa tofauti bali ni katiba yenye maudhui
na malengo tofauti dhidi ya binadamu,katiba ambayo itajali haki, kweli,
na katiba ambayo itajali demokrasia.
Kuhusu
urafiki wao na CUF wakati hapo awali kulikuwa na vijembe vya hapa na
pale amesema kuwa urafiki wao umeunganishwa na malengo ya msingi ambayo
malengo hayo ni katiba iliyo bora yenye malengo mazuri,misingi mizuri
iliyojaa uadilifu nchi itakuwa na amani.
Lema
amesema kuwa Ukawa haitaishia kwenye bunge la katiba bali utafika mbali
zaidi na hatimaye mwaka 2015 mahali amabpo CHADEMA watasimamisha
mgombea NCCR MAGEUZI hawatasimamisha vivyo hivyo kwa chama cha CUF.
Kutafuta
haki kuna njia nyingi, hivyo Njia ya kupata katiba iliyobora hapa
Tanzania ni pamoja na maandamano, mikutano ya hadhara, ama kuandamana
ili kufikisha ujumbe dunia kwamba kinachoendelea bungeni sio sahihi.
Sambamba
na hayo Lema ameongeza kuwa Ukawa inataka Katiba mpya itakayo kataa
ufisadi, itakayotatua kero za muungano,itakayotambua haki za binadamu
mahakamani na polisi, itakayotambua maslahi bora ya wananchi wake,
itakayolinda utu wa binadamu katika taifa lake , itakayo mpunguzia rais
madaraka yake, Katiba ambayo Mawaziri hawata kuwa wabunge, pamoja na
kutokuwepo kwa wakuu wa wilaya na mikoa.
CHANZO: MJENGWA BLOG