MTU
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA WLLIAM KABINJI (38) MKAZI WA KIJIJI
CHA MANTENGU [A] ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI
KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA SEHEMU ZA USONI NA JUU YA JICHO LA
KUSHOTO KISHA KUNYONGWA SHINGO NA KUTUNDIKWA JUU YA MTI AKIWA AMEFUNGWA
SHINGONI KWA KUTUMIA KITENGE.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.06.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA
KATIKA KIJIJI CHA ILEMBO, KATA YA VWAWA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA
MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KULIPIZA
KISASI BAADA YA MAREHEMU KUCHOMA MOTO NYUMBA TATU ZA JIRANI ZAKE NA
KUITEKETEZA KABISA NYUMBA YA ELIAS MWAMLIMA (32) MKAZI WA KIJIJI CHA
MANTENGU [A] TAREHE 04.06.2014 MAJIRA YA SAA 21:30 USIKU NA KUTOROKA.
JITIHADA ZA KUWASAKA NA KUWAKAMATA WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AMBAO NI MAJIRANI WANAOFAHAMIKA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA
KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA
MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA
KWA MIGUU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA EZEKIEL KYANDO (72) MKAZI WA
BAGAMOYO AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA
MAKANDANA – TUKUYU KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA GARI NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.06.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI
KATIKA ENEO LA BAGAMOYO TUKUYU MJINI, KATA YA BAGAMOYO, TARAFA YA TUKUYU
KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.
UCHUNGUZI UNAONYESHA KUWA CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA
ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI HIYO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA NONDE
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SAMSON JULIUS (18) AKIWA NA BHANGI KETE 68
SAWA NA UZITO WA GRAMU 340.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 08.06.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA
ENEO LA STENDI KUU YA MABASI, KATA NA TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA
BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YAKO
Imetolewa na:
(AHMED Z. MSANGI – SACP)
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.