SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 9, 2014

Msichana ang'atwa na kuchomwa na pasi na mwajiri wake.

Picha:Kelele za vilio jana zilisimamisha kwa muda shughuli katika Wodi ya Wanawake ya Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam baada ya mama mzazi wa msichana, Yusta Lucas (20) anayedaiwa kuteswa kwa kung’atwa na kuchomwa kwa pasi mwili mzima kumwona mwanawe kwa mara ya kwanza.
Binti anayedaiwa kuteswa kwa kung’atwa na kuchomwa kwa pasi na mwajiri wake, Yusta Lucas (kushoto) akilia pamoja na mama yake, Modesta Simon katika Hospitali ya Mwananyamala jana, baada ya mama yake kuwasili kutoka Tabora ili kumjulia hali. Picha na Venance Nestory     


Hali ya msichana Yusta Lucas mwenye umri wa miaka 20 aliyefanyiwa ukatili wa kufungiwa ndani kwa zaidi ya mwaka mmoja huku akipewa adhabu ya kunga'twa na kuchomwa kwa pasi na mwajiri wake Amina Maige wa Mwananyamala jijini Dar es salaam inaendelea vizuri kufuatia matibabu anayopata ya majeraha yaliyomsababisha kupoteza fahamu.