SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, June 20, 2014

KIKWETE AKABIDHI BODABODA 10 KWA UWAPA ARUSHA

President Jakaya Kikwete
RAIS wa jamhuri ya muungano waTanzania, Dakta,Jakaya Kikwete

Mahmoud Ahmad Arusha
RAIS wa jamhuri ya muungano waTanzania, Dakta,Jakaya Kikwete,jana alikabidhi msaada wa Pikipiki10 kwa chama cha Akiba na Mikopo cha Waendesha Pikipikikatika jiji la Arusha,UWAPA SACCOS, zenye thamani ya shilingi milioni 15.9.
Pikipiki hizo zimekabidhiwa kwa uongozi wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Jiji la Arusha (UWAPA) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi yake ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa waendesha boda boda hao wakati akihutubia mkutano wa hadhara Novemba mosi mwaka 2012 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa ziara ya Mkoa wa Arusha Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo amesema ajali za pikipiki mkoani humo zimepungua kutokana na waendesha pikipiki hizo kupewa mafunzo na hivyo kuzingatia sharia za usalama bara barani tofauti na hapo awali.


Amewapongeza waendesha bodaboda hao , kwa kuanzisha vituo vyao ambavyo kwa sasa vinafahamika na tayari vimeshasajiliwa na kuwataka waviimarishe katika swala zima la ulinzi na usalama wa abiria.

Mulongo, amesema kuwa waendesha boda boda hao wamekuwa wakichangia sana kuimarisha maswala ya usalama na hivyo matukio makubwa ya uhalifu yamepungua sanjari na matukio ya kujichukulia sharia
mkononi.

Amesema msaada huo ni mtaji wa kuendeleza Saccos hiyo ,na akaahidi kuwanunulia Jacket 1000 ambazo ni sale ili watambulike .

Mulongo,akawataka wasijihusishe na vurugu ,wasikubali kugeuzwa kuwa ni sehemu ya kufanya vituko na vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani.

Pia aliwataka wasikubali kutumiwa na kugeuzwa nabaadhi ya watu ili wasitumbukie na kushabikia mamboyasiyofaa kwa jamii ikiwemo uhalifu .

Akisoma lisara, Katibu wa Uwapa Saccos, Salvatory Massawe, amesema Sacoss hiyo ina wanachama 2300 na bado milango iko wazi kwa waendesha boda boda wengine jijini Arusha kujiunga,kwa kuwa Saccos hiyo ni kiungo muhimu .

Amesema kuwa tayari vituo 144 vimesajiliwa na bado mchakato wa kusajili vituo vingine unaendelea lengoni ili viutambulike na kufahamika hivyo inakuwa ni rahisi kuzuia matukio ya kihalifu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Saccos hiyo, Godlight Rugemarila, alisema kuwa,boda boda zimetoa ajira nyingi na hivyo kupunguza kwa kiwango kikubwa matukio ya uhalifu.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na Wilaya ya Arusha,watumishi katika Sekretarieti ya Mko huo na Watendaji wa Jiji la Arusha.