Nahodha wa timu ya mpira wa pete ya Business Times Limited akikabidhiwa kikombe mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa.
Nahodha
wa timu ya mpira wa pete ya Business Times Limited akikabidhiwa kitita
cha shilingi milioni 4 baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia
(mwenye traksuti nyeusi) akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya mpira
wa miguu ya Business Times Limited baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa
wa mpira wa miguu. Wengine ni viongozi wajuu wa NSSF wakishuhudia.
Nahodha
wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited akionesha kitita
cha shilingi milioni 4 na Nusu mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa
wa mpira wa miguu. Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited akionesha kombe juu mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi. Baadhi
ya wachezaji wa Business Times Limited wakishangilia kikombe na kitita
cha shilingi milioni 4 na Nusu mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa
wa mpira wa miguu.
Nahodha wa Timu ya Mwananchi kulia akipokea kombe kutoka kwa mgeni rasmi, kikombe hicho ni cha mshindi wa nne.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Abubakar Rajabu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi. Mwakilishi
wa mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Juma Nkamia (mwenye traksuti nyeusi) akitembelea banda la NSSF
lililopo kwenye mashindano hayo kupata maelezo anuai. Meza
kuu ikifuatilia mechi anuai za fainali ya Mashindani ya 11 ya NSSF
yanayoshirikisha vyombo vya habari anuai katika mchezo wa mpira wa miguu
na mpira wa pete kwa wasichana.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Changamoto wakipata picha na kikombe chao cha mshindi wa pili mpira wa miguu.
Mechi ya fainali kati ya Business Times Limited na Habari ya Zanzibar mpira wa pete ikiendelea. Meza kuu ikifuatilia mechi za fainali ya Timu ya mpira wa pete kutoka Habari, Zanzibar ikipata picha ya ukumbusho. Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited (wenye jezi bluuu) ya wakilisha
CHANZO: NA ANKAL MICHUZI
WAZIRI wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala
amelipongeza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa
kuviunganisha vyombo vya habari anuai nchini Tanzania kupitia tasnia ya
michezo.
Dk.
Mukangala ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika hotuba yake
iliyosomwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Juma Nkamia kwa niaba ya waziri, alipokuwa akifunga rasmi
Mashindani ya 11 ya NSSF yanayoshirikisha vyombo vya habari anuai katika
mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete kwa wasichana.
Dk.
Mukangala alisema kwamba mashindano hayo yamekuwa yakivikutanisha vyombo
anuai vya habari kutoka Tanzania Bara na Visiwani hivyo kujenga
uhusiano mzuri kwa washiriki kupitia michezo, huku yakiimarisha uhusiano
kati ya vyombo hivyo na shirika la NSSF ambalo hudhamini mashindano
hayo kila mwaka kwa muda wa miaka 11 mfululizo hivi sasa.
"...Hakuna
ubishi kwamba miaka 11 sio michache kwa kuendesha mashindano kama haya,
lakini kwa sababu uongozi wa NSSF unaheshimu na kukubali nafasi ya
vyombo vya habari katika kuelimisha jamii ni wazi kwamba mtaendelea
kutenga bajeti ya mashindano haya kila mwaka," alisema Dk. Mukangala.
Aidha
aliwapongeza washindi wa mwaka huu kwa jitihada na nidhamu ya mchezo
waliozionesha hadi kufanikiwa kutwaa ushindi, hivyo kuwataka wanahabari
wote kuendelea kuyatumia mashindano hayo kwa kujenga mahusiano mazuri na
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii.
Mwaka
huu timu ya Kampuni ya Bussnes Times Limited (BTL) imefanikiwa kutwaa
kombe la mpira wa miguu na kuzawadiwa fedha shilingi milioni nne na nusu
baada ya kuishindilia Changamoto mabao matatu kwa mtungi, nafasi ya
pili ilichukuliwa na timu ya Changamoto na kujinyakulia kikombe pamoja
na kitita cha shilingi milioni tatu na nusu.
Mshindi
wa tatu mpira wa miguu imeibuka timu ya wenyeji wa mashindano hayo NSSF
baada ya kuifunga timu ya Mwananchi, hata hivyo NSSF walichukua kikombe
na kusamehe kitita chao cha shilingi milioni 2 kilichokabidhiwa mshindi
wa nne, yaani Timu ya Mwananchi.
Neema
ya mashindano hayo mwaka huu iliiangukia kampuni ya BTL ambapo kwa
upande wa mpira wa Pete pia timu ya wasichana ya kampuni hiyo
ilifanikiwa kutwaa ubingwa na kukabidhiwa kombe na fedha shilingi
milioni 4, nafasi ya mshindi wa pili imechukuliwa na timu ya Habari
kutoka Zanzibar na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni tatu na
nusu.
Washindi
wa tatu mpira wa pete imeibuka timu ya NSSF ambao walitwaa kombe bila
fedha ambazo zilichukuliwa na mshindi wa nne (Mwananchi). Kikombe cha
nidhamu kimenyakuliwa na timu ya Tumaini wamiliki wa Redio na TV Tumaini
pamoja na gazeti la Tumaini Letu.
Jumla
ya timu 20 za mpira wa miguu na 18 za mpira wa pete zimeshiriki
mashindano hayo kwa mwaka huu idadi ambayo inazidi kuongezeka kila mwaka
tangu kuanza kwa mashindano hayo.
Hafla
ya kufunga mashindano hayo iliyofanyika katika viwanja vya Sigara (TCC)
jijini Dar es Salaam pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya NSSF, Abubakar Rajabu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk.
Ramadhani Dau viongozi waandamizi wa shirika la NSSF pamoja na wageni
mbalimbali waalikwa.