Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali na Mafunzo katika semina hiyo
--
Na Arusha yetu Blog
IMEELEZWA kuwa Watanzania ni
wavivu wa kusoma Majarida mbali mbali yanayoweza kuwaongezea upeo ukilinganisha
na nchi zingine.
Hayo yamebainishwa na Mmoja wa
maafisa wa Jarida la Mkulima Mbunifu, Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya,
wakati akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari za kilimo na wataalamu
wa kilimo yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Arusha Crown ya Mjini hapa.
Ameongeza kuwa kunatofauti
kubwa ya Mwitikio wa kusoma machapisho kati ya Raia wa Tanzania ukilinganisha
na Kenya ambako imeelezwa kuwa wanauhitaji mkubwa wa kujifunza mbinu mpya za
kilimo tofauti na Watanzania ambao hawana uhitaji wa kusoma na kutaka kujua
zaidi.
Akieleza Mikakati ya Jarida la
Mkulima Mbunifu mmoja katika ya Maafisa wa Jarida hilo, Caroline Nyakundi kutoka
Nchini Kenya, amesema tangu kuzinduliwa kwa jarida hilo Juni,2011 limeonesha
mwitikio mkubwa kutokana na kupata taarifa nyingi kutoka kwa wakulima
wakilihitaji ili kujua zaidi habari za Kilimo.
0 comments:
Post a Comment