Mark Zuckerberg
Mwanzilishi
wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa amezungumza na Rais Barack
Obama kumwelezea kero lake kuhusu udukuzi unaofanywa na serikali kwa
mitambo ya Dijital.
Zuckerberg
mwenye umri wa miaka 29, amesema kuwa serikali ya Marekani inapaswa
kupigia debe internet badala ya kuwa adui wa mitandao ya kijamii.
Matamshi
yake yanakuja siku moja baada ya ripoti kuwa shirika la ujasusi la
Marekani ilibuni mtandao bandia wa Facebook ili kuweza kuvamia mitambo
ya Kompyuta inayotumiwa kwa uchunguzi.
Shirika la NSA lilisema kuwa taarifa hiyo sio ya kweli.
Mnamo mwezi Septemba, Zuckerberg alisema kuwa Marekani ilikosea sana taarifa zilipoibuka kuwa inafaya udukuzi kwenye mitandao.
Mwanateknolojia huyo alisema kuwa huenda ikachukua muda mrefu sana kwa mageuzi yoyote kufanyika.
Zuckerberg
alisema, alisema "wakati wahandisi wetu wanapofanya kila hali kuboresha
usalama kwenye mtandao, kwetu ni kama tunawalinda kutokana na wahalifu
kwenye mitandao, sio serikali yetu.''
"Serikali
ya Marekani lazima ipigie debe Internet sio kuwa adui wa mtandao.
Lazima waelezee wanachokifanya la sivyo, watu hawatakuwa na imani tena
na serikali.''
Shughuli
za shirika la ujasusi la Marekani lilijipata motoni baada ya ufichuzi
kutolewa na aliyekuwa jasusi wakati mmoja Edward Snowden, mwaka jana.
Ufichuzi
wake ulionyesha kuwa shirika hilo lilikuwa linakusanya taarifa za simu
za watu, kufanya udukuzi na kuvamia mitandao ya watu.
Chanzo BBC Swahili
Chanzo BBC Swahili