TAARIFA YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA
UBUNGE JIMBO LA CHALINZE .FABIAN LEONARD SKAUKI –
MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI –CUF DHIDI YA MATHAYO MANG’UNDA
TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO -CHADEMA
13.03.2014
--
Mimi FABIAN L. SKAUKI, mgombea ubunge wa uchaguzi
mdogo jimbo la CHALINZE kwa Ticket ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea
Pingamizi mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa sababu
zifuatazo.
1.
Ndugu MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za
uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa
sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi
gani.
2.
Ndugu MATHAYO .M. TORONGEY amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika
Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui kusoma
wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba amedanganya na amepoteza
sifa za kuwa mgombea.
3.
Ndugu MATHAYO .M.TORONGEY amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini,ambao
amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea. Ambapo katika
fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na zile
zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba sahihi zote hizi
zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika. Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea
kuwa mgombea.
4.
Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY ameshindwa kutimiza
mahitaji ya kisheria ya kuwa na wadhamini wasiopungua 25, badala yake
amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali
wa jimbo la CHALINZE, na kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.
Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao
kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
Majina ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya
kisheria na namba zao ni
JINA LA MDHAMINI
NAMBA YA KADI KURA
1.
HABIBU ALLY SAIDI
* 16886275*
2.
MOHAMMED RAMADHANI *30376567*
3.
ABDULKADIR ALLY
*49264905*
4.
SHABANI SULEYMAN *16984045*
5.
JUMA MRISHO
*48759563*
6.
RAJABU ALLY *16872368*
7.
MANENO MIRAJI *16872059*
Wananchi
wenye namba na majina hayo hapo juu waliojazwa kama wadhamini kuanzia namba 1
hadi 7 kwenye fomu yake hawana sifa za kupiga kura kwenye maeneo ambayo
wamejazwa wanatokea.
Hii ni
kutokana na ukweli kwamba idadi halali ya wadhamini wanaobaki ukiwaondoa hao
saba watabaki 21, hawakizi vigezo vya kuwa wadhamini.
5.
Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY amedanganya Uraia wake, na kwamba yeye si Mtanzania wa kuzaliwa ndio
maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia wake. Hivyo anakosa sifa ya kuwa
mgombea.
Hivyo
ninaomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa mgombea wa chama cha demokrasia na
maendeleo (CHADEMA) ndugu
MATHAYO.M.TORONGEY kwa kuwa anakosa sifa
za yeye kuendelea kuwa mgombea.
Wako katika ujenzi wa Taifa
FABIAN LEONARD SKAUKI
……………………………………………………..
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE.